Spain ni moja ya nchi zilizo na maambukizi ya virusi hivyo, ikiwa nyuma ya Marekani na Itali kwa idadi ya maambukizi.
Tangazo hilo la Jumatano lilitoa idadi ya vifo hivi sasa nchi spain kuwa zaidi ya 9,000.
Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona duniani Jumatano imefikia 870,000, vifo zaidi ya 43,000, na watu zaidi ya 184,000 wamepona baada ya maambukizi hayo.
Tukielekea katika bara la afrika, taarifa ya shirika la habari la AFP inasema hadi sasa Zaidi ya maambukizi elfu 5 na 700 yameripotiwa katika bara hilo pamoja na vifo 190.
Afrika
Burundi ambayo ni miongoni mwa mataifa mawili yaliokuwa bado kuguswa na corona barani Afrika, Jumanne nchi hiyo iliripoti maambukizi ya kwanza ya watu 2.
Lakini wataalamu wa afya wanaendelea kuonya kwamba hali yaweza kuwa mbaya zaidi katika nchi nyingi barani Afrika kutokana na migogoro inayoendelea, usafi duni, makazi duni ya mijini na hospitali zisizo na vifaa vya kutosha. Mfano jamuhuri ya Afrika ya kati yenye raia million 4.7na inayo vifaa vinne pekee vya kusaidia wagonjwa kupumua.
Nayo Ethiopia imechukua uamuzi wa kuahirisha uchaguzi mkuu ambao ulikuwa unatarajiwa kufanyika tarehe 29 August mwaka huu kutokana na mlipuko wa corona.
Wakati huo huo Marekani inaendelea kuongoza kwa maambukizi yaliyokuwa yamefikia zaidi ya 188,000 muda mfupi uliopita, huku kukiwa na vifo zaidi ya 4000. Taarifa ya leo imesema watu zaidi ya elfu 7,200 wamepona kutokan na maambukizi ya corona nchini Marekani.
Italy ndilo taifa la bara la Ulaya ambalo linazidi kuhangaika kukabilianana janga la corona. Takwim za kitengo cha dunia kinachofuatilia maambukizi ya corona zaonyesha kuwa idadi ya vifo imezidi 12,400 muda mfupi uliopita, huku maambukizi yakizidi laki 170,000.
China kuliko anzia ugonjwa huo, viongozi wameripoti leo maambukizi mapya 7 pekee, ikionekana kuwa taifa hilo limepiga hatua kubwa kwa kudhibiti mlipuko huo.
Saudi Arabia
Afisa wa ngazi ya juu wa Saudi Arabia amewataka wale wanaopanga kwenda hija kuahirishwa uamuzi huo kwa hivi sasa.
Mahujaji wako katika maandalizi ya kwenda Saudi Arabia kutoka nchi zote ulimwenguni ifikapo mwisho wa mwezi Julai kutekeleza ibada ambayo ni lazima kwa mwenye uwezo na afya kutekelezamara moja uhai wa kila Muislam.
Lakini kutokana na janga la virusi hivyo, na Saudi Arabia kupiga marufuku kuingia miji ya Makka na Madina, Waziri wa masuala ya hija na umra Muhammad Saleh bin Taher Banten amekiambia kituo cha televisheni cha taifa watu wasubiri mpaka hali itakapo kuwa inaeleweka zaidi mustakbali wake.
Marekani
Nchini Marekani, maafisa wanasema Wamarekani lazima wajiandae kuwepo kwa uwezekano wa vifo kati ya 100,000 hadi 240,000 vinavyotokana na virusi vya corona, wakati akisisitiza kuendelea kufuata agizo lililokuwepo la kuepukana misogamano au kutokuwa karibu na mtu mwengine ili kutoa nafasi ya fursa bora zaidi ya kupunguza vifo hivyo.
Dkt Anthony Fauci, mkurungenzi wa Kituo cha Taifa cha Maradhi ya hasasia na maambukizi Marekani amesema anamatumaini idadi hiyo haitofikia kiwango hicho cha juu, lakini kiuhalisia wa mambo watu ni lazima wawe tayari kupokea habari hizo.
Nchi zote duniani zimesitisha shughuli zote katika miji mikuu, mikoa na hata taifa zima kujaribu kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.
Moja kati ya nchi zilizotoa katazo la hivi karibuni kusitisha shughuli zote isipokuwa zile muhimu ni Vietnam, amri iliyoanza kutekelezwa Jumatano.
New Zealand
Wiki iliyopita, New Zealand ilifunga migahawa, mabaa, ofisi na shule. Waziri Mkuu Jacinda Ardern alisema Jumatano ni mapema mno kusema ni kwa kiasi gani hatua hizo zilizochukuliwa zimesaidia hadi sasa na akasisitiza kuwepo upimaji zaidi kwa ajili ya kugundua maambukizi na kuzuia kuenea kwa maambukizi mapya.
Serikali ya New Zealand imeripoti wagonjwa wapya 61 ambayo imepelekea idadi ya maambukizi ya nchi hiyo kufikia 708.
Korea Kusini
Huko Korea Kusini, ambako upimaji wa virusi vya corona kwa taifa umesaidia kudhibiti kiwango cha maambukizi nchini, maafisa wameripoti maambukizi mapya ya watu 101 Jumatano. Nchi hiyo imeanza kutekeleza amri mpya ya karantini ya siku 14 kwa kila mtu anayeingia nchini.
China
Hatari ya maambukizi yanayoletwa na watu kutoka nje ya nchi ambayo inarudisha nyuma mafanikio ya kudhibiti kuenea kwa COVID-19 katika jamii kumefanya hatua kama hii kuchukuliwa na China, ambayo kwa miezi kadhaa ilikuwa ikiongoza duniani kwa maambukizi ya virusi vya corona, lakini hivi sasa imekuwa ni nchi inayotoa matumaini ambapo kidogo kidogo wameanza kuondoa katazo la watu kukaa majumbani.
Ujerumani
Ujerumani, maafisa wa afya wamesema kulikuwa na wagonjwa wapya 5,500 ikifanya nchi hiyo iwe njiani muda sio mrefu kuwa nchi ya pili kuipita China kwa maambukizi.