Iwapo hilo litatokea basi huenda mlipuko utakaporejea virusi hivyo vikawa na nguvu kubwa zaidi ya maambukizi iwapo tahadhari zinazo stahiki hazitachukuliwa.
Akizungumza jioni Jumatano wakati wa mkutano wa kila siku wa kutoa taarifa juu ya virusi vya corona White House, Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Uchunguzi wa Maradhi ya Hasasia na Yanayo Ambukiza Dkt Anthony Fauci amesema wagonjwa wenye maambukizi wameanza kujitokeza katika nchi ya Afrika Kusini na nyingine zilizoko kusini mwa dunia ambako hivi sasa zinaingia katika kipindi cha baridi.
Ameeleza iwapo mlipuko mkubwa utatokea katika maeneo hayo, itakuwa ni dalili tosha kuwa virusi hivyo vinaweza kuwa vya misimu na nchi za Kaskazini ya dunia wajiandae kwa mlipuko wa mara ya pili wa virusi hivyo mwakani.
Fauci amesema hilo linaweka mkazo zaidi juu ya haja ya kuendelea kutafuta chanjo ambayo itakuwa tayari iwapo duru ya pili ya maambukizi ya virusi vya corona itatokea, pamoja na kuwa na orodha ya dawa ambazo zinaweza kutibu na silama kwa matumizi ya wagonjwa wanaopata virusi hivyo.