Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:53

Waziri Pompeo aanza juhudi za kuwasuluhisha Ghani na Abdullah Afghanistan


Mtendaji mkuu wa zamani Abdullah Abdullah (kushoto) na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani.
Mtendaji mkuu wa zamani Abdullah Abdullah (kushoto) na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amewasili mjini Kabul Jumatatu ikiwa ni ile ziara iliyokuwa haijatangazwa ya juhudi za kusuluhisha mgogoro wa kisiasa kati ya Rais Ashraf Ghani na hasimu wake Abdullah Abdullah.

Mgogoro huo umekuwa ukitishia kuharibika kwa makubaliano yaliyo sainiwa kati ya Marekani na Kikundi cha Taliban mwezi Februari.

Ghani na Abdullah walijitangaza kuwa marais wan chi hiyo baada ya uchaguzi uliokuwa na mvutano.

Ziara hiyo, imekuja wakati viongozi wa ulimwengu wamepunguza safari za nje kwa sababu ya janga la kimataifa la maambukizi ya virusi vya corona, na wakati msimamizi anayewakilisha mazungumzo kwa niaba ya uongozi wa Rais Trump nchini Afghanistan Zalmay Khalilzad amekuwa mjini Kabul kwa wiki kadhaa akijaribu kusaidia kumaliza matatizo hayo ya kisiasa, anaendelea kujadili kiini cha mgogoro huo na pande zote husika.

“Tunachotaka ni Rais Ghani na mtendaji mkuu wa zamani Abdullah wafikie makubaliano ya namna ya kuunda serikali ya pamoja inayokubalika na pande zote,” afisa mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amewaambia waandishi wa habari.

“Pande zote zinatambua kuwa kuna mpasuko. Tuangalie kama wataweza kufikia suluhu leo.”

Wakati huohuo baada ya wiki kadhaa za kutoelewana, serikali ya Afghan na Kikundi cha Taliban walifanya mazungumzo ya moja kwa moja Jumapili wakitumia mtandao wa video wa Skype kujadili suala la kuachiwa kwa wafungwa.

Mkutano huo wa kifundi uliochukuwa zaidi ya masaa mawili leo ulikuwa muhimu sana, makini na wa kina. Nashukuru pande zote husika katika mazungumzo hayo. Kila mtu anaelewa vilivyo tishio la virusi vya corona linalofanya kuachiwa kwao kuwa ni jambo la dharura,” amesema Khalilzad katika ujumbe wake wa Twitter, mwakilishi maalum wa Marekani katika suluhu ya Afghanistan.

Suala la kuachiwa kwa wafungwa takriban 5000 kwa kubadilishana na takriban wafanyakazi wa usalama wa Afghanistan 1000 limekuwa likuzuia kuanza kwa mazungumzo kati ya Taliban na vikundi vingine vya Afghanistan ambavyo ilikuwa uanze Machi 10 kwa mujibu wa makubaliano yaliyo sainiwa kati ya Marekani na Kikundi cha Taliban huko Doha mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG