Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:25

Watu kumi wauawa katika milipuko wa mabomu Afghanistan


Ramani ya Afghanistan
Ramani ya Afghanistan

Milipuko ya mabomu mawili tofauti imetokea mapema Jumanne nchini Afghanistan na kuuwa takriban watu 10 wakiwemo watoto pamoja na kujeruhi wengine 18.

Mashambulizi hayo yametokea siku chache baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kusema kuwa licha ya viwango vyake vibaya Afghanistan, mwaka 2019, umekuwa mbaya zaidi kwa watoto, huku taifa hilo likitajwa kuwa hatari zaidi miongoni mwa mengine yanayoshuhudia mapigano.

Maafisa wa Afghanistan wamesema kuwa bomu moja kando ya barabara mapema leo limelipua gari lililobeba raia kwenye jimbo la kusini mashariki la Khost ambapo takriban watu 10 wameuwawa.

Gavana wa Jimbo Halim Fidai amesema kuwa wanawake watatu na watoto wawili ni miongoni mwa waliokufa kwenye shambulizi katika wilaya ya Alisher.

Fidai ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba waathirika wa shambulizi hilo walikuwa wakielekea kwenye mazishi ya mwanafamilia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Afrghanistan Nasrat Rahimi amelaumu Kundi la Taliban kutokana na matukio hayo.

XS
SM
MD
LG