Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:54

Shambulio la bomu laua watu 63 na kujeruhi 183 Afghanistan


Wahanga wa shambulio la bomu mjini Kabul wakizikwa katika kaburi la pamoja, Afghanistan, Agosti 18, 2019. (AP Photo/Rafiq Maqbool)
Wahanga wa shambulio la bomu mjini Kabul wakizikwa katika kaburi la pamoja, Afghanistan, Agosti 18, 2019. (AP Photo/Rafiq Maqbool)

Kikundi cha Islami State cha Afghanistan kimedai kuhusika na shambulio la bomu katika harusi mjini Kabul lililoua watu 63 na kujeruhi wengine 183.

Wahanga hao wa mlipuko uliotokea usiku katika harusi iliyokuwa imejaa watu walikuwa wengi wao ni wafuasi wa jumuiya ya waliowachache Mashia wa tawi la Hazara.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Afghanistan Nasrat Rahimi alithibitisha mauaji hayo katika tamko lilitolewa mapema Jumapili, akisema kati ya wahanga hao kulikuwa na watoto na wanawake.

Shambulio hilo limetokea wakati kundi la Taliban na serikali ya Marekani wajaribu kujadili makubaliano ya Marekani kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistan, ili kundi la Taliban lifanye mazungumzo ya kutafuta amani na serikali ya Afghanistan ambayo inaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Kundi la Taliban limekanusha kuhusika na shambulio hilo na kulaani vitendo hivyo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG