Hizo ni juhudi za serikali yake katika kukomesha mgogoro hatari unaoongezeka nchini humo na kutafuta suluhisho la pamoja katika kukubaliana na ugaidi kutoka katika mipaka ya nchi hiyo.
Serikali imemtaja juhudi mpya ya eneo ikiwa ni mkutano wa “mchakato wa Kabul” lakini mkutano huo wa kwanza unafanyika wakati hali ya usalama wa taifa ikiendelea kuwa mbaya sana na mvutano mkubwa wa kisiasa kuongezeka.
Amesema jirani za nchi ya Afghanistan, kama vile Iran and Pakistan, ni kati ya nchi zilizothibitisha kuhudhuria.
Msemaji huyo amesema pia nchi nyingine zitakazo hudhuria mkutano huo ni Marekani, Russia, India, Saudi Arabia, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE), Uingereza, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ahmad Shakeb Mustaghani amewaambia waandishi Jumatatu kuwa serikali haiko tayari kuruhusu changamoto za nchi hiyo kuzotesha juhudi hizo za mazungumzo.
“Na vyombo vyetu vya usalama vimeihakikishia serikali kuweka ulinzi wa kutosha kwa ajili ya kuhakikisha usalama wakati mkutano unafanyika,” amesema Mustaghani.
Matukio ya wiki iliyopita, yamegubika kile kilichoelezewa hatua muhimu ya kuendeleza juhudi za amani na usalama nchini Afghanistan.
Watu wawili walijitoa muhanga na maadamano ya hatari dhidi ya serikali mjini Kabul yameuwa takriban watu 120 na kujeruhi watu 600 zaidi.
Hali ya umwagaji damu ilianza na shambulizi la mabomu yaliyokuwa kwenye lori yaliyolipuka katika eneo la wanadiplomasia katika mji mkuu huo Jumatano, May 31.