Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:26

Wataliban wadai kuhusika na mlipuko uliouwa raia 35


Wafanyakazi wa manispaa wakisafisha eneo lilipotokea mlipuko Kabul, Julai 24, 2017.
Wafanyakazi wa manispaa wakisafisha eneo lilipotokea mlipuko Kabul, Julai 24, 2017.

Mtaliban mmoja amejitoa mhanga Jumatatu kwa kujilipua ndani ya gari na kuuwa watu wasiopungua 35 na kuwajeruhi dazeni zaidi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani huko Afghanistan, Najib Danish amethibitisha vifo hivyo.

Ameeleza kuwa mtu huyo alijitoa mhanga baada ya kuendesha gari lake lililojaa milipuko na kugonga basi moja dogo lililojaa raia ambao ni wafanyakazi wa serikali huko magharibi mwa mji huo.

Mlipuko huo ulitokea wakati basi likipita kwenye eneo la soko lililojaa watu na kusababisha vifo kwa wauzaji maduka na wapiti njia, walioshuhudia wamewaambia waandishi wa habari.

Maafisa wa hospitali wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka. Msemaji wa Kabul ameiambia VOA kwamba waathirika wengi walikuwa waajiriwa wa kiwanda cha madini na mafuta.

Wapiganaji wa Taliban mara moja walidai kuhusika na kupanga tukio hilo, wakidai kuwa mlipuaji wao alikusudia kulipua mabasi madogo mawili yaliyokuwa yamebeba maafisa wa usalama wa Afghan, na 38 kati yao wameuawa.

Rais wa Afghan Ashraf Ghani amelaani shambulizi hilo kwa raia na kusema ni la kusikitisha na lilofanywa na watu waoga.

Shirika la Kimataifa la Haki za binadamu (Amnesty international) limelaani shambulizi hilo lilolenga raia na kusema kuwa ni sawa na uhalifu wa kivita na kutaka serikali ya Afghan ihakikishe inawalinda raia wake.

XS
SM
MD
LG