Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:43

Wahanga 35 wazikwa katika kaburi moja Afghanistan


Wananchi wa Afghanistan wakiomboleza vifo vya ndugu na jamaa zoa.
Wananchi wa Afghanistan wakiomboleza vifo vya ndugu na jamaa zoa.

Wanakijiji na ndugu zao upande wa mashariki wa Afghanistan Jumamosi walichimba kaburi mmoja na kuwazika waathiriwa 35 waliouwawa Ijumaa katika shambulizi la kujitoa muhanga kwa bunduki na bomu katika msikiti wa Mashia.

Mwandishi wa VOA huko Afghanistan amesema mamia ya waombolezaji walihudhuria maziko hayo yaliyoandaliwa chini ya ulinzi mkali katika eneo la Gardez, mji mkuu wa Jimbo la Paktia, ambako mauaji hayo yalifanyika.

Watoto watatu ni kati ya wale waliouwawa. Mkurugenzi wa afya wa jimbo hilo, Walayat Khan Ahmadzai, alithibitisha Jumamosi kuwa shambulizi hilo liliwajeruhi zaidi ya watu 90 na hali ya watu wengine 17 ni “mahtuti.”

Polisi na wale walioshuhudia wamesema watu wawili waliojitoa muhanga waliokuw wamefunika nyuso zao, na wakiwa na silaha aina ya rifle, walishambulia msikiti uliokuwa umefurika wakati wa sala ya mchana katika eneo la Khawaja Hasan wa makao makuu ya jimbo hilo.

Washambuliaji hao waliingia katika eneo la msikiti na kuwapiga risasi waliokuwa wakifanya ibada kabla ya kujitoa muhanga wao wenyewe, mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Raz Mohammad Mandozai ameiambia VOA.

Mara baada ya tukio hilo hapakuwa na madai ya kuhusika kwa shambulizi hilo la kumwaga damu huko Paktia, ambayo iko mpakani na Pakistan.

Msemaji wa kikundi cha upinzani cha Taliban mara moja alikanusha kikundi hicho kuhusika na shambulizi hilo msikitini, na kusababisha tuhuma hizo kuelekezwa kwa kikundi cha Islamic State huenda kikawa kimehusika na mauaji hayo ya Mashia ya kinyama.

Tawi la Afghan linalo fungamana na kikundi cha magaidi cha Mashariki ya Kati, kinachojulikana kama ISK-P kimedai kuhusika na takriban mashambulizi yote ya hivi karibuni dhidi ya maeneo ya ibada ya Mashia na mikusanyiko mbalimbali Afghanistan.

Rais Ashraf Ghani na Mtendaji Mkuu Abdullah Abdullah wote wamelaani vikali shambulizi hilo la kigaidi lililofanywa kwa wananchi waliokuwa wanafanya ibada wasiokuwa na hatia.

XS
SM
MD
LG