Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:02

CDC yasema Afrika lazima ijitayarishe kukabiliana na janga la corona


 Wajumbe wa Bodi ya CDC Afrika wakiwa na maafisa wa Umoja wa Afrika.
Wajumbe wa Bodi ya CDC Afrika wakiwa na maafisa wa Umoja wa Afrika.

Nchi tatu za Africa zinamaambukizi zaidi katika mlipuko wa virusi vya corona bara la Afrika, lakini naibu mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga Afrika wanasema bara lote lazima lichukue hatua.

Virusi hivyo vinasababisha taharuki katika maeneo mengine ya dunia na sisi katika bara la Afrika ni lazima tujitayarishe ili isiweze kutuathiri kwa idadi kubwa kama ilivyo katika bara la Ulaya na Asia, kwa sababu mifumo yetu ya afya haiwezi kuhimili maambukizo kama hayo,” Dr Ahmed Ogwell ameiambia VOA kupitia mawasiliano ya mtandao wa Skye kutoka Addis Ababa, Ethiopia.

Kwa hivyo, mkakati uliobora zaidi, na ule ambao wanashauri serikali iufuate, amesema, “ni kujikinga na kupunguza madhara ambayo yatasababishwa na virusi hivyo kwa bara la Afrika.”

Ogwell amesema taasisi yake, ambayo ni shirika la ushauri wa kifundi la Umoja wa Afrika, anashirikiana na AU kuzijengea uwezo wa utayari nchi mbalimbali katika maeneo makuu matatu, ikiwemo kuboresha utoaji tahadhari katika bandari za nchi hizo na mahospitali; kuongeza utaalamu wa kuweza kupima kirusi COVID-19, ambao tayari nchi 43 wanauwezo huo; na kujenga uwezo wa kuzuia maambukizi na kudhibiti hali hiyo ili wagonjwa wenye maambukizi waweze kuwekewa karantini na kufuatiliwa.

Hadi sasa, nchi zilizo athirika vibaya sana Misri ikiwa na maambukizi 196, Afrika Kusini 116 na Algeria 73. Kuna maambukizi 605 katika bara lote hadi kufikia Machi 18.

Ogwell amesema kitu kizuri pamoja na kuwepo janga hili nchi hizi tatu zina mifumo iliyomadhubuti ya afya na uwezo wa kufanya vipimo. Lakini, kuongezeka kwa maambukizi kunaweza kuielemea nchi yoyote.

XS
SM
MD
LG