Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:28

Shirika la ndege la Flybe lafilisika baada ya kupoteza wasafiri


Shirika la ndege kubwa zaidi la Uingereza ni muathirika wa hivi karibuni kibiashara kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Flybe ilikuwa imeokolewa ikiwa karibu kutetereka mwezi Januari lakini hatimaye limefilisika Alhamisi.

Kufilisika huku ni baada ya kuwa haina wasafiri na abiria wengi kufuta safari zao kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona unaosababishwa na kirusi cha Covid-19. Uingereza ilikuwa imeripoti idadi ya maambukizo inayokaribia watu 100 mpaka Alhamisi.

Flybe ilikuwa inatoa huduma zake hasa Uingereza na viwanja vya ndege vya Ulaya kuliko katika vituo vya uwanja wa ndege vikubwa. Kuanguka kwa shirika hilo kunaonekana ni kikwazo kwa juhudi za serikali kuboresha kuunganisha safari na kusawazisha tena uchumi wa Uingereza.

“Tunamasikitiko kwa kweli, ni sikitiko kwa kweli,” mfanyakazi wa Flybe Katherine Denscham alisema hayo wakati akijiandaa kuondoka kazini katika uwanja wa ndege wa Exeter kusini magharibi ya Uingereza.

Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA) imetahadharisha Alhamisi kuwa sekta nzima ya usafiri wa anga duniani imeathiriwa na wimbi kubwa la kupungua idadi ya wasafiri.

“Tulishuhudia kuathirika kwa mapato yanayozidi dola za Marekani bilioni 100, hayo ni takriban mapato kutokana na asilimia 19 ya wasafiri wa kimataifa. Kwa hiyo hii itakuwa ni kutetereka kwa mapato yanayokaribia kiwango cha kipindi cha mzozo wa kifedha ulioikabili dunia,” Mchumi mwandamizi wa IATA Brian Pearce amewaambia waandishi wa habari huko Singapore.

XS
SM
MD
LG