Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:59

Idadi ya vifo kutokana na kirusi corona yafikia 900, maambukizo 40,000


Wanafunzi wa Indonesia wakiwa wamevalia maski wakiwasili kutoka Guangzhou, China, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa China Outbreak Soekarno-Hatta, Indonesia, China, Alhamisi Jan. 30, 2020
Wanafunzi wa Indonesia wakiwa wamevalia maski wakiwasili kutoka Guangzhou, China, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa China Outbreak Soekarno-Hatta, Indonesia, China, Alhamisi Jan. 30, 2020

Idadai ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa kirusi corona nchini China imepindukia 900 Jumatatu na idadi maambukizo kufikia zaidi ya watu 40,000.

Maafisa wa China wanasema kwa siku ya Jumapili peke yake watu 97 walifariki wakati Wachina wakirudi makazini Jumatatu baada ya sherehe za mwaka mpya inayofuata hisabu ya kuandama mwezi.

Maafisa hao wanaendelea kuchukuwa hatua za kukabiliana na mlipuko huo ambao Shirika la Afya Duniani linasema huenda ugonjwa huo umeanza kupunguza kasi licha ya kwamba idadi ya vifo vinaongezeka .

Rais wa China Xi Jinping alionekana akiwa amevalia maski akitembelea mtaa mmoja wa Beijing Jumatatu na hospitali moja iliyopangwa kuwapokea wale waloambukizwa na virusi vya corona.

Kiongozi huiyo alipimwa joto la mwili wake na kuzungumza na wakazi wa mtaa wa Anhuali Xi, na kuwaambia wananchi inabidi kuwa na imani ya uwezo wetu wa kuushinda ugonjwa huyo.

Ugonjwa huo umeshauwa zaidi ya watu 900 hivi sasa huku mataifa kote duniani yakiendelea kuchukuwa hatua za kukabiliana na mlipuko huo.

Wakati huo huo meli ya kitali iliyotia nanga katika mji wa Yokahama imeripoti kesi mpya 66 mapema Jumatatui ikiwa ni mara dufu ya idadi ya watu waloripotiwa kuambukizwa wiki iliyopita.

Benki kuu ya China imetangaza kwamba imetenga dola bilioni 43 za kusaidia biashara zitakazovkabiliwa na matatizo kutokana na mlipuko huo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG