Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:56

China : Vifo kutokana na kirusi corona vimefikia watu 81


Makundi mbalimbali Hong Kong wanashinikiza mpaka kati yao na China Bara ufungwe.
Makundi mbalimbali Hong Kong wanashinikiza mpaka kati yao na China Bara ufungwe.

Idadi ya vifo kutokana na maambukizo ya kirusi corona imeongezeka na kufikia 81 Jumatatu.

Wagonjwa wengine 3,000 wamethibitishwa kuwa na maambukizo, wakati serikali ikiongeza muda wa mapumziko kwa siku tatu katika sherehe za mwaka mpya unaofuata kuandama kwa mwezi.

Wakati huohuo biashara kubwa nchini humo zimefungwa au waajiriwa kupewa muongozo wa kufanyia kazi majumbani mwao katika juhudi za kupunguza maambukizo.

Waziri Mkuu Li Kequang alitembelea mji wa Wuhan katika kituo cha mlipuko wa kirusi hicho.

Serikali inaongeza juhudi za kupambana na ugonjwa unaosababishwa na kirusi corona huku kukiwa na shutuma kutoka kwa wananchi ya kutokuwepo na uwajibikaji wa kutosha.

Idadi ya watu walioathiriwa na kirusi hicho China imepanda kwa asilimia 30 kutoka ile ya awali huku nusu yao wakitokea jimbo la Hubei ambao mji mkuu wake ni Wuhan.

Lakini baadhi ya wataalamu wanasema idadi ya walioathiriwa inaweza kuwa kubwa zaidi.

Hali hiyo imesababisha sherehe za mwaka mpya kuahirishwa hadi February 2 ambapo watu wengi husafiri kuingia na kutoka China.

Wawekezaji wana wasiwasi kuhusu matokeo ya safari, utalii na harakati za kiuchumi huko China kwa hivi sasa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG