Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:54

Jopo la ushauri la WHO latathmini mlipuko wa Ebola Uganda


Wafanyakazi wa afya wanaowahudumia wagonjwa wenye virusi vya Ebola wakiwa katika vazi linalowalinda na maambukizi nchini Uganda
Wafanyakazi wa afya wanaowahudumia wagonjwa wenye virusi vya Ebola wakiwa katika vazi linalowalinda na maambukizi nchini Uganda

Shirika la Afya Duniani, WHO, huenda likatangaza hali ya dharura ya kimataifa kwa mlipuko wa ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, ambao hivi sasa umesambaa na kuingia nchini Uganda, watalaamu wamesema kuwa jopo la ushauri katika WHO limekutana hivi leo Ijumaa.

Mlipuko huo mbaya ni wa pili kwa ukubwa tangu ule wa Afrika Magharibi mwaka 2014 mpaka 2016. Mlipuko huu umesababisha maambukizi 2,084 na vifo 1,405 tangu utangazwe mwezi August mwaka jana.

WHO ilisema siku ya Alhamisi kwamba watu waliofariki nchini Uganda walikuwa wakitokea nchini Congo na wameingia Uganda tayari wakiwa na ugonjwa huo.

Jopo la wataalamu 13 katika kamati ya dharura ya WHO (EC) walikutana Ijumaa mchana kutathmini ushahidi wa karibuni na kuona kama kuna haja ya kuutaja ni dharura ya kimataifa ya afya.

Uamuzi kama huo unaweza kuboresha hatua za afya ya umma, ufadhili na rasilimali na huenda ukajumuisha mapendekezo kuhusu masharti yakusafiri na biashara, watalaamu na makundi ya misaada wamesema.

Watu bado wanafariki nje ya vituo vya matibabu ya ebola, na kuzifanya familia kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huo na wengi wao hawamo katika orodha ya watu ambao wanafuatiliwa na watalaamu wa afya, amesema Lawrence Gostin, Profesa wa afya ya umma ulimwenguni katika chuo kikuu cha Georgetown kilichopo Washington DC.

“Chanjo haziwezi kufanya kazi peke yake kama jamii zitaficha kesi kwa sababu ya kutoaminiana. Ghasia nazo zinaendelea kuwepo. Tuko na suala hili kwa muda mrefu ujao,” Gostin amesema na kuzungumzia mashambulizi mabaya kwa vituo vya afya nchini Congo.

Jopo, ambalo mara mbili liliamua kutotangaza dharura, litatoa mapendekezo kwa mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye atafanya maamuzi ya mwisho.

Dharura nne tu zimetangazwa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita: vitui vya H1 ambavyo vilisababisha mlipuko wa mafuta mabaya sana mwaka 2009, mlipuko wa ebola Afrika Magharibi, ugonjwa wa polio mwaka 2014 na virusi vya Zika mwaka 2016.

Afisa wa juu wa WHO, Mike Ryan amesema Alhamisi hakuna kesi zinazojulikana za maambukizo ya ebola ya mtu kwa mtu nchini Uganda na kwamba kuna dalili za kutia moyo nchini Congo, ambako kusambaa kwa maradhi hayo kumeonyesha kupungua kasi katika miji ya Butembo na Katwa. Hata hivyo virusi hivi sasa viko katika maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na huko Mabalako, amesema.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG