Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:19

Uganda imethibitisha kuna kesi moja ya Ebola nchini humo


Wafanyakazi wa afya wakiwa wamemshikilia mtoto aliyeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola huko Beni, DRC mwaka 2018
Wafanyakazi wa afya wakiwa wamemshikilia mtoto aliyeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola huko Beni, DRC mwaka 2018

Kesi hiyo ni ya mtoto raia wa kongo aliyewasili Uganda siku ya Jumapili na familia yake na amewekwa eneo maalum ndani ya hospitali mjini Kasese iliyopo kwenye mpaka wa magharibi wa Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo-DRC

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kwamba mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano amepimwa na kupatikana na virusi vya Ebola ikiwa ni mara ya kwanza kwa virusi hivyo kuenea kuvuka mipaka ya kitaifa wakati wa kile ambacho kinaonekana kuwa mlipuko wa pili mkubwa kutokea katika historia ya ugonjwa huo.

Mtoto huyo raia wa kongo aliwasili Uganda siku ya Jumapili na familia yake na amewekwa katika eneo maalum ndani ya hospitali mjini Kasese iliyopo kwenye mpaka wa magharibi wa Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo-DRC.

Wafanyakazi wa afya na juhudi za kutoa chanjo ya Ebola huko DRC, 2018
Wafanyakazi wa afya na juhudi za kutoa chanjo ya Ebola huko DRC, 2018

Habari hizo ni pigo kwa wafanyakazi wa afya Kongo ambao wamekuwa kwa miezi kadhaa wakipambana kuzuia kusambaa kwa virusi vya Ebola kutoka nchini Kongo ambako kuna zaidi ya watu 2,000 waliorodheshwa kuwa wameambukizwa virusi hivyo katika muda wa miezi 10 iliyopita na takribani watu 1,400 kati yao wamefariki.

Wizara ya afya na shirika la afya dunia wameshapeleka timu ya dharura hadi Kasese kuwapima watu wengine ambao huwenda wako katika hatari ya kuambukizwa na kufuatilia kwa karibu matukio katika mji huo.

XS
SM
MD
LG