Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:01

WHO inasema kuna mafanikio katika kupambana na Ebola huko DRC


Mfanyakazi wa huduma ya afya akitoa chanjo ya Ebola kwa mkazi wa jimbo la kivu kaskazini
Mfanyakazi wa huduma ya afya akitoa chanjo ya Ebola kwa mkazi wa jimbo la kivu kaskazini

Maambukizo ya ugonjwa huo yamepungua kwa kiasi kikubwa katika wiki kadhaa zilizopita katika mji wa Butembo na Katwa ambao ndio kiini cha mlipuko japokuwa changamoto bado zipo

Shirika la afya Duniani-WHO lilisisitiza Jumanne juu ya maendeleo iliofanya katika kupambana dhidi ya ugonjwa wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC lakini ilionya kwamba changamoto bado ipo.

Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO, Dr. Matshidiso Moeti alimulika matukio ya usalama katika kiini cha mlipuko wa Ebola huko mashariki ya Congo ambapo alieleza wafanyakazi wa afya watano wamekufa akiwemo daktari wa WHO.

Wakati huo huo mkuu wa huduma za dharura wa WHO, Dr. Michael Ryan aliwaambia waandishi wa habari kuwa ufuatiliaji wa ugonjwa huo umeimarika hata kama idadi ya mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa afya iliongezeka kwa mara tatu katika kipindi cha miezi mitano iliyopita. Ryan aliendelea kusema kwamba WHO ilifanikiwa kuboresha uangalizi wa utendaji katika viwango vya kesi zisizokuwepo kwenye orodha.

Maambukizo ya ugonjwa huo yamepungua kwa kiasi kikubwa katika wiki kadhaa zilizopita katika mji wa Butembo na Katwa ambao ndio kiini cha mlipuko japokuwa changamoto bado zipo.

XS
SM
MD
LG