Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:55

UN itasimamia utokomezaji wa Ebola huko DRC


Wafanyakazi wa afya wakiwa mji wa Beni, Septemba 2018
Wafanyakazi wa afya wakiwa mji wa Beni, Septemba 2018

Ripoti kuhusu idadi ya vifo vinavyotokana na Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC inaeleza kwamba tangu mwezi Agosti mwaka 2018 zaidi ya watu 1,200 wameshakufa na wengine kadhaa wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo

Umoja wa Mataifa sasa ndio utasimamia harakati za kupambana na ugojwa wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC ili kuhakikisha unatokomeza kabisa ugonjwa huo ambao hadi sasa umeshawaua watu wengi na huku kukiwa na hatari ya kusambaa katika nchi jirani.

Hatua hiyo ya kuiomba Umoja wa Mataifa usimamie juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ebola zimechukuliwa huko Geneva kufuatia ongezeko la vifo vya kila mara vya Ebola katika eneo la Kivu kaskazini pamoja na Ituri huko mashariki mwa DRC kwenye mji wa Butembo mahala ambako kumeshuhudiwa vifo na maambukizi mengi kwa wakazi wa huko.

Akizungumza na mwandishi wa VOA mbunge wa Beni, Kizerbo Kasereka alieleza kwamba alipokea kwa furaha taarifa za Umoja wa Mataifa kuingilia kati kusimamia utokomezaji wa ugonjwa wa Ebola katika eneo lao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00

XS
SM
MD
LG