Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:02

WHO yachukuwa hatua za haraka kukabiliana na Ebola Uganda


Wafanyakazi wa afya wanaokabiliana na Ebola wakiwa wanavalia mavazi ya kujikinga na Ebola katika majaribio wanayofanya kila wiki huko hospitali ya Bwera mpakani na DRC, magharibi ya Uganda, on Disemba. 12, 2018.
Wafanyakazi wa afya wanaokabiliana na Ebola wakiwa wanavalia mavazi ya kujikinga na Ebola katika majaribio wanayofanya kila wiki huko hospitali ya Bwera mpakani na DRC, magharibi ya Uganda, on Disemba. 12, 2018.

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeripoti kuchukuwa hatua za haraka kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Ebola nchini Uganda, huku hatua za madhubuti zikichukuliwa kuhakikisha kwamba watu wanaoishi kwenye mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaanza kupokea chanjo dhidi ya Ebola

Hadi sasa, visa vitatu vya maambukizi vimethibitishwa ikiwemo kifo kimoja.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa shirika la afy aduniani WHO, nchini Uganda Irene Nakasiita, inaeleza kwamba wataalam wa kupambana na ebola wametumwa katika wilaya ya Kasese, mpakani na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kuweka mikakati ya dharura kuzuia virusi vya ebola kusambaa kwa umma.

Hii ni baada ya mtoto mvulana mwenye umri wa miaka mitano kuaga dunia, siku moja baada yake na familia yake kutembelea watu wa ukoo wa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Shirika la afya duniani limesema ripoti za Ebola nchini Uganda ni za kutisha, lakini kwa ushirikiano na wizara ya afya ya Uganda, wamekuwa wakieka mikakati ya kujitayarisha dhidi ya ugonjwa huo, na kwamba kinachofanyika kwa sasa, ni kuimarisha mikakati iliyopo kwa kuwshirikisha wadau mbali mbali wakiwemo shirika la msalaba mwekundu.

Waziri wa afya wa Uganda Jane Ruth Aceng, amesema chanjo dhidi ya ebola katika wilaya ya Kasese na sehemu zilizo karibu, itaanza kutolewa ijumaa hii.

“Wizara ya afya, shirika la afya duniano na kituo cha kukabiliana na magonjwa ya kuambikaza, wataanza kutoa chanjo dhidi ya ebola kwa watu wanaoaminika kuwa karibu na visa vilivyothibitishwa kabla ya chanjo kutolewa kwa uma, kuanzia juni 14.

Chanjo hii ni salama na ombi letu ni kwa watu kushirikiana na maafisa wa afya, uhamiaji na usalama kuzuia ebola kusambaa hadi sehemu zingine za nchi”, amesema waziri Aceng.

Watu wanane waliokaribiana na mtoto aliyeaga dunia wakiwemo wazazi wake, na jamii waliotembelea DRC, wanachunguzwa. Ndugu mdogo na bibi ya marehemu mwenye umri wa miaka 50 wamethibitishwa kuambukizwa.
Pikama Ram, ni mkaazi wa wilaya ya Kasese.

“Watu wana wasiwasi sana kwa sababu tupo mpakani na watu wanavuka mpaka kutoka kila upande bila kujua ni nani mgonjwa na nani si mgonjwa. Tunajua Congo imeathiriwa sana na Ebola na hivyo nasi tupo katika hatari ya kuambukizwa.

Lakini kuna wengine ambao bado hawajakubali kwa sababu ya kiwango kidogo cha elimu. Wanasema vipimo vya serikali si vya kweli,” amesema Wilayani Kasese, shughuli za sokoni zimepigwa marufuku, sawa na mikusanyiko ya watu kama sherehe za harusi, mazishi na mikutano ya ukumbini.
Marufuku imetolewa ya watu kugusana, kusalimiana, huku maafisa wa mpakani wakiimarisha ukaguzi wa watu wanaovuka mpaka.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington DC.

XS
SM
MD
LG