Eneo hilo limegubikwa na vita kwa miaka mingi, na wakazi wengi wa eneo hawana imani na watu wageni, hata wale ambao wanajaribu kuzuia kuenea kwa virusi hatari vya Ebola, imeripotiwa na mwandishi wa VOA akiwa makao makuu ya WHO, Geneva.
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (UN) imeripoti kuwa matukio ya uvunjifu wa amani mashariki mwa DRC yameongezeka kwa wingi katika miezi michache iliyopita.
Hadi sasa mwaka huu, imeripotiwa kuwepo mashambulizi 174 yaliofanywa na vikundi venye silaha Kivu Kaskazini yakilenga vituo vya afya, wafanyakazi na wagonjwa. Hii ni pamoja na vifo vya watu watano na majeruhi 51.
Katikati ya mwezi April, Daktari kutoka Cameroon Richard Mouzoko alipigwa risasi na kuuawa wakati akitoa huduma hospitalini huko Butembo, Kivu Kaskazini. Tukio hilo
Jumamosi iliyopita, wanakijiji walimuua mfanyakazi wa afya katika sekta ya afya huko Mabalako.
Mkurugenzi wa WHO wa eneo la Afrika, Matshidiso Moeti, amesema wafanyakazi wa afya wanatishiwa maisha na watu wenye silaha na wanaishi kwa hofu, wakiwa hawajui siku gani nyingine mashambulizi yatafanyika.
Anasema hali hii ya ukosefu wa usalama unapelekea kutoweza kufika maeneo yenye maambukizi na inaongeza idadi ya wagonjwa walioambukizwa.