Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:19

Chanjo ya Ebola yafanyiwa tathmini ili ianze kutumika Afrika Mashariki


Mfanyakazi wa afya akiwa katika kituo cha matibabu ya Ebola Beni, mashariki ya DRC, Aprili, 16, 2019.
Mfanyakazi wa afya akiwa katika kituo cha matibabu ya Ebola Beni, mashariki ya DRC, Aprili, 16, 2019.

Wakati timu za wanaokabiliana na Ebola wakihangaika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mawaziri wa afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanasema wanatambua hatari zake na wanatathmini kuanza kutumia chanjo ya Ebola iliyoko katika majaribio.

Katika kipindi cha hivi karibuni, vituo vinavyo tibu Ebola DRC vimekuwa vikishambuliwa na hivyo wafanyakazi wanaokabiliana na ugonjwa huo wameshindwa kufikia maeneo yenye milipuko.

Vyanzo vya habari Afrika Mashariki vimeripoti kuwa hivi sasa nchi sita, hasa zile zilizoko mpakani na majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri nchini DRC, ambako milipuko ya ugonjwa huo iliendelea kwa kasi, wanakabiliana na vikwazo vyote kuhakikisha wanaweza kwa ufanisi kufikisha matibabu pale ambapo imethibitishwa Ebola ipo.

Uganda, Burundi na Rwanda ni maeneo yaliyo na hatari kubwa ya maambukizi, wakati baadhi ya sehemu za Sudan Kusini na Tanzania ambayo yako karibu na miji iliyoko mpakani yanakabiliwa na hatari ya wastani ya maambukizo hayo.

Gazeti la The East African limemnuku Kaimu Mkuu wa Idara ya Afya kwenye Sekretarieti ya EAC Arusha, Dr Michael Katende akieleza uamuzi wa kutumia chanjo ya Ebola.

Amesema ni jambo la busara kuwakinga wafanyakazi walioko mstari wa mbele kukabiliana na ugonjwa huu pamoja na wilaya zinazokabiliwa na tishio la maambukizi.

“Ilivyokuwa ni kinga ambayo inaonyesha matumaini zaidi kuliko nyingine, ni bora kuwa na kitu ambacho kinakupa kinga kuliko kutokuwa na kinga yoyote kabisa,” amesema.

XS
SM
MD
LG