Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:43

Madaktari, vifaa, madawa vya wasili eneo la mlipuko wa Ebola


Wauguzi wanaofanya kazi na shirika la Afya Duniani wakitoa chanjo kwa wananchi kuzuia kuenea katika mji wa Mbandaka Mei 21, 2018 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Ebola.
Wauguzi wanaofanya kazi na shirika la Afya Duniani wakitoa chanjo kwa wananchi kuzuia kuenea katika mji wa Mbandaka Mei 21, 2018 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Ebola.

Timu ya madaktari imewasili mjini Beni, Kivu kaskazini Alhamisi ambako tayari kuna wagonjwa wanne wenye virusi vya Ebola tayari kukabiliana na mlipuko mpya wa Ebola.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa madaktari, madawa na vifaa tayari vimepelekwa katika eneo hilo.

Sampuli za wagonjwa hao zilipelekwa Jumatatu kupimwa na kuthibitishwa kuwepo kwa virusi vya Ebola.

Gavana Julien Paluku, wa Kivu Kaskazini alitangaza mlipuko huo Jumatano kwenye ukurasa wake wa tweeter ikiwa ni wiki moja tu baada ya maafisa wa Umoja wa mataifa na serikali ya Kongo kutangaza kumalizika kwa mlipuko huo ambao uliuwa watu 33.

Virusi vya Ebola vilithibitishwa katika jimbo la Kivu Kaskazini Paluku aliandika katika ukurasa wake wa tweeter. Natoa wito wa utulivu na uangalifu.

Maafisa wamesema sasa wanahisi wamejiandaa vizuri zaidi kupambana na Ebola ikiwa ni tofauti kubwa na mlipuko wa 2014 ambao uliuwa zaidi ya watu 11,000 hasa Guinea, Liberia na Sierra Leone. Ili kuzuia mlipuko huu wa hivi karibuni wafanyakazi wa huduma walisambaza dawa ya chanjo ya majaribio yenye nguvu kwa mtu yeyote aliyegusana na wale walioathirika.

Gavana Paluku amesema kwamba serikali inayo madawa na chanjo, lakini imeomba washirika wa afya duniani ikiwemo shirika la afya duniani (WHO) kuendelea kuwasaidia katika kukabiliana na mlipuko huo mpya wa Ebola.

Ebola imetokea kivu kaskazini, wiki moja baada ya serikali ya DRC kutangaza kwamba ugonjwa huo uliojitokeza mwezi Mei katika jimbo la Equateur ulizimwa baada ya kuuwa watu zaidi ya 30.

XS
SM
MD
LG