Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:20

Wasiwasi endapo Ebola itaingia Butembo


Wafanyakazi wa afya wakiwa wamevalia nguo maalum za kujikinga na virusi vya Ebola, mjini Beni, Kivu Kaskazini, DRC, Septemba 5, 2018.
Wafanyakazi wa afya wakiwa wamevalia nguo maalum za kujikinga na virusi vya Ebola, mjini Beni, Kivu Kaskazini, DRC, Septemba 5, 2018.

Mgonjwa mmoja wa Ebola kutoka Beni inaripotiwa kuwa amefariki katika mji wa Butembo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wenye wakazi takriban milioni 1.

Kwa mujibu wa afisa wa Shirika la Afya Duniani Peter Salama kifo hicho kimethibitishwa na ameeleza kuwa habari njema ni kuwa mlipuko huu umejulikana kwa haraka na juhudi za kuudhibiti zinaendelea.

Pamoja na juhudi hizi maafisa wa afya wana wasiwasi kuwa mlipuko huo katika eneo la Mashariki ya DRC, unaweza kuenea kwa kasi, pamoja na kugunduliwa kwa haraka na juhudi zinazo endelea kufanyika.

Wizara ya Afya imesema Jumanne mlipuko huo uliodumu kwa wiki tano umeuwa watu 85, na kuwaambukiza watu 124 ambao tayari wameripotiwa, kati yao 93 wakiwa wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Jambo linalotia wasiwasi zaidi ni ripoti za wagonjwa wawili huko Butembo, mji ulioko kilomita 60 kutoka sehemu ambayo ni kitovu cha mlipuko huo.

Hilo ni lenye kutia wasiwasi kwa sababu Butembo ni kituo kikuu cha biashara ambacho ni karibu na mpaka wa Uganda ambao ni makazi ya takriban watu milioni moja.

Pia wagonjwa hao 13 waliotambulika hivi karibuni, maafisa wa afya wanasema hawajui nini kimesababisha maambukizo hayo pamoja na juhudi kubwa ya kufuatilia kila mgonjwa aliyeletwa ambaye alikuwa amegusana na watu ambao walikuwa na maambukizi ya ugonjwa huo hatarishi.

XS
SM
MD
LG