Hatua hiyo inalenga kukabiliana na ongezeko la maambukizo ya Ebola nchini humo na kushambuliwa kwa maafisa wa afya..
Vyanzo vya habari vinasema kuwa wakazi wa eneo la mashariki mwa DRC wamewashambulia maafisa wa afya na kukataa kushirikiana na serikali katika juhudi za kupambana na mlipuko wa Ebola ambao inaaminika kuwa umeuwa watu 118 tangu mwezi Julai 2018.
Ebola imesambaa hadi mji wa Beni, wenye maelfu ya watu na kuambukiza watu kadhaa.
Maafisa wanasema kwamba hawawezi kufaulu katika kukabiliana na ugonjwa huo iwapo hakuna ushirikiano kutoka kwa raia, huku kisa kimoja au viwili, vya maambukizi mapya, vikiripotiwa kila siku.