Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:12

WHO yasema kuna ongezeko la maambukizo ya Ebola DRC


Wahudumi wa afya wakiendelea kukabiliana na Ebola DRC.
Wahudumi wa afya wakiendelea kukabiliana na Ebola DRC.

Shirika la Afya Duniani (WHO) na maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanaripoti kuwa kuna ongezeko la idadi ya walio ambukizwa ugonjwa wa Ebola katika siku chache zilizopita.

Sio chini ya watu 177 wamethibitishwa au wanahisiwa kuwa na maambukizo katika upande wa Mashariki mwa DRC mpaka kufikia siku ya Jumamosi – hilo ni ongezeko kutoka maambukizi 162 yaliyo rikodiwa Jumanne iliyopita. Hivi sasa kuna maambukizo 11 yanayo shukiwa kuwepo wakati uchunguzi wa vipimo unaendelea kufanyika.

Mpaka sasa watu wasio pungua 113 wamepoteza maisha katika mlipuko wa ugonjwa huu, wakwanza kutokea upande wa Mashariki ya DRC.

Baadhi ya vifo vya hivi karibuni vimetokea nje ya hospitali, jambo ambalo linaongeza hatari ya kuenea kwa ugonjwa huu. Jamii nyingi zina desturi ya kuzika ambapo wanaoomboleza wanagusa miili ya wapenzi wao na kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Juhudi za kudhibiti mlipuko huo unasuasua kwa sababu ya vitisho vya kutokuwepo usalama vinavyo sababishwa na vikundi vya wapiganaji kadhaa, jamii kutokuwa na imani na wahudumu wa afya na jografia ya kusambaa kwa virusi. Shirika la Afya lina wasiwasi kuwa virusi hivyo vinaweza kuenea katika nchi za jirani ya DRC.

XS
SM
MD
LG