Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:12

China yasema uwezo wa kirusi corona kuenea unaongezeka


Mfanyakazi wa afya akipima joto la mwili wa msafiri aliyekuwa anaingia katika stesheni ya treni za mjini jijini Beijing, Jumapili, Jan. 26, 2020.
Mfanyakazi wa afya akipima joto la mwili wa msafiri aliyekuwa anaingia katika stesheni ya treni za mjini jijini Beijing, Jumapili, Jan. 26, 2020.

Kasi ya maambukizo ya kirusi corona inaongezeka na kuna uwezekano idadi ya wagonjwa ikaongezeka pia, Kamisheni ya Afya ya Taifa ya China imesema Jumapili.

Wakati huohuo watu zaidi ya 2,000 wameambukizwa duniani na 56 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Kirusi hiki, kinaaminika kuwa kilianza katika soko la bidhaa za baharini mwishoni mwaka 2019, katikati ya Jiji la Wuhan, China ambalo lilikuwa linauza nyama ya porini.

Kirusi hiki kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, hadi Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, na Canada.

Jumapili, China ilitangaza nchi nzima katazo la kuuza nyama ya porini katika masoko, migahawa na mitandao ya kieletroniki ya biashara.

Waziri wa Kamisheni ya Afya ya Taifa Ma Xiaowei, akizungumza na vyombo vya habari, amesema uwezo wa serikali wa kufahamu kirusi hiki kipya ni finyu na hawajui hatari zinazoweza kuambatana na kubadilika kwa kirusi hiki.

Ma amesema muda ambao kirusi hiki cha corona kinachukuwa hadi kujitokeza ni kati ya siku mmoja hadi 14, na kuwa kirusi hiki kinaambukiza hata wakati kinajijenga mwilini, kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa homa kali ya mafua, SARS, kirusi corona kilichoibuka China na kuua takriban watu 800 duniani mwaka 2002 na 2003.

Juhudi za kudhibiti maambukizi, ambayo imehusisha katazo la usafirishaji na kusafiri na kusitisha matukio ya sherehe kubwa, utaongozeka, amesema Ma, wakati akizungumza na waandishi wa habari wengi waliojitokeza siku ya pili ya mapumziko ya mwaka mpya unaotumia hisabu ya mwezi.

XS
SM
MD
LG