Shirika hilo limesema pamoja na kuwa virusi hivyo vimeenea katika nchi jirani ya Uganda, sababu ni kuwa vilihamishwa na familia iliyokuwa na maambukizo.
Uamuzi huo wa ufuatiliaji wa karibu unafuatia ushauri wa kamati ya dharura ya WHO ambayo hukutana kurejea milipuko hatari zaidi ya magonjwa ambukizi duniani.
Mkuu wa shirika la afya la UN Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye yuko DRC kuangalia harakati za kukabiliana na Ebola, amesema anakubaliana na ushauri huo wa kamati.
“Ilivyokuwa mlipuko huo kwa wakati huu siyo tishio kwa afya ya dunia, nataka kusisitiza kuwa kwa familia na jamii zilizoathirika na ugonjwa huu, mlipuko wa Ebola ni suala la dharura,” Tedro amewaambia waandishi wa habari.
Pia ametoa wito fedha ziongezwe kwa ajili ya kupambana na hali hii tata iliyojitokeza, ambayo imerikodi zaidi ya wagonjwa 2,000 ikiwemo zaidi ya vifo 1,400, tangu ugonjwa huu ulipojitokeza mashariki ya DRC Agosti 2018.