Watu 89 walikufa kutokana na kirusi corona Jumamosi, Kamisheni ya Afya ya Taifa ya China imesema Jumapili asubuhi.
Ugonjwa wa mapafu uliokuwa hatari SARS inaaminika kuwa uliuwa watu zaidi ya 774 na kusababisha watu 8,100 kuugua nchini China na mkoa maalum wa uongozi wa Hong Kong.
Kamisheni hiyo imeripoti kuwa maambukizo mapya yalipungua siku ya Jumamosi kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari 1, kufikia 2,656, ikiwa hivi sasa ni jumla ya maambukizo 37,198.
Joseph Eisenberg, Profesa wa magonjwa ya milipuko katika Shule ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Michigan, ameiambia Shirika la Habari la Reuters ilikuwa mapema mno kusema iwapo mlipuko wa kirusi corona ndio unatia kasi kwa sababu ya kutokuwepo uhakika wa idadi kamili ya wagonjwa.
“Hata kama idadi ya wagonjwa walioripotiwa ikiwa inaongezeka, hatujui kile kinachoendelea na wajonjwa wale ambao hawajaripotiwa,” ameiambia Reuters. Hili hasa ni tatizo katika baadhi ya maeneo zaidi ya vijijini.”
Wakati huo huo taarifa iliyotolewa Jumapili na Shirika la Afya Duniani, WHO, inasema, hata hivyo, kuna dalili za maambukizi ya kirusi hicho cha corona kuanza kudhibitiwa.
Takwimu za WHO zinaonesha kiwango cha maambukizo kimepunguwa kwenye mji wa Hubei, ambao ndio kitovu cha kirusi cha corona, lakini imeonya kuwa bado idadi ya wanaopoteza maisha inaweza kuongezeka.
Pia Hong Kong imetangaza abiria wote 3,600 pamoja na wafanyakazi waliokuwa wamewekwa karantini katika meliya World Dream, wataruhusiwa kuondoka.
Vyanzo vya habari Hong Kong vimesema vipimo vilivyo kuwa vimechukuliwa vya abiria 1,800 vimeonyesha hawana maambukizi.