Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:32

Masharti yatolewa na serikali mbalimbali kwa safari za China


Stadium yageuzwa kuwa hospitali ya muda huko Wuhan
Stadium yageuzwa kuwa hospitali ya muda huko Wuhan

Mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu kutokana na virusi vya Corona huko China unasababisha serikali na taasisi mbali mbali kuweka masharti ya kutembelea China na mashirika ya ndege kusitisha safari zao.

Wakati huohuo miji mikubwa ya China ya Bejing na Shanghai ikiripotiwa kuwa haina harakati zozote wakati wasi wasi ukiongezeka baada ya serikali kuwataka watu kubaki nyumbani kutokana na kuongezeka kwa vifo idadi rasmi ikiwa imefikia 490 na maambukizo ya ugonjwa huo kufikia watu 27,000.

Watu wamebakia majumbani katika mji mkuu wa China, Bejing wenye wakazi milioni 22 baada ya wakuu wa serikali kuwataka wafanye hivyo na kutangaza kuendelea kwa sikukuu ya mwaka mpya inayotumia hisabu ya mwezi hadi Februari 9.

Idadi ya vifo yafikia 490

Maafisa wa China wanasema hatua hiyo inachukuliwa kutokana na idadi ya vifo kuongezeka kufikia watu 64 kufariki kwa siku moja na kufikisha idadi ya vifo 490, vingi vikitokea katika jimbo la Hubei lililozuiliwa usafiri wa aina kuingia au kutoka.

Mji mkuu wa biashara wa China wa Shanghai nao umesitisha shughuli zake zote na wakazi wanahofia kuporomoka kwa uchumi.

Yi Huida mkazi wa Shanghai anasema anadhani ugonjwa utakua na athari kubwa kwa biashara nchini humo.

Yi Huida mkazi wa Shanghai anaeleza : "Ninadhani biashara zote hazitafanya viziuri mnamo robo ya kwanza ya mwaka 2020. Ninatumaini mambo yataweza kubadilika baadae, lakini hata iwapo biashara zitafunguliwa kila mtu anaogopa kutoka nje.

Soko la hisa la Shanghai limeshuhudia kuporomoka kwa bei za hisa kwa kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha miaka minne hapo Jumatatu na kuendelea kupata hasara ya karibu asili mia 2 hadi hii leo.

WHO ni dharura ya kitaifa

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetangaza ugonjwa huo wenye dalili za kama homa kuwa ni dharura ya kimataifa, lakini siku ya Jumanne ikasema haujafikia kiwango cha janga ingawa umeenea katika mataifa mengi zaidi.

Mkurugenzi wa idara ya kujitayarisha dhidi ya mambukizi ya kimataifa kwenye WHO Sylie Briand anasema wanafanya kila njia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Sylvie Briand, Mkurugenzi wa kuzuia mambukizi WHO anasema : "Kwa hivi sasa hatujafika kiwango cha janga la kimataifa. Tuko katika awamu ya dharura kukiwepo na mambukizo katika maeneo mbali mbali na tunajaribu kuzia kuenea kwa uambukizaji."

WHO ilitangaza pia itawasiliana na mashirika ya ndege na kampuni za utalii wiki hii kutoa ushauri wa namna ya wafanyakazi wao wanaweza kujikinga na uambukizaji. Shirika hilo linaendelea kuhimiza kuendelea kwa usafiri na biashara na China.

Ushauri wa WHO

Jumanne wakurugenzi wakuu wa WHO walikutana na kutoa ushauri wa kuzitaka nchi zote duniani kushirikiana katika kupashana habari na kubadilishana takwimu juu ya virusi vya Corona. Oliver Morgan mkurugenzi wa kutathamini dharura za afya anasema wameanza kufahamu jinsi ugonjwa unasamba kutoka mtu mmoja hadi mwengine.

Oliver Morgan mkurugenzi wa kutathmini dharura za Afya anasema : "Hivi sasa tunafahamu bayana jinsi mtu mmoja anavyomuambukiza mwengine nje ya china. kuna watu 27 wanaoripotiwa kuambukizwa na mtu mwenginhe katika mataifa 9."

Hayo yakiendelea Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la kimataifa IMF mashirika mawili makuu ya fedha duniani yameeleza Imani yano na nguvu za uchumi wa china licha ya wasiwasi unaojitokeza.

Hata hivyo mataifa mbali mbali ya dunia yanachukua tahadhari kuzuia ugonjwa usienee zaidi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG