Hii ni katika juhudi za kutafuta ufumbuzi kwa kile wakosoaji wa mfumo wa sasa hivi wanasema ni upungufu wa vituo vya upimaji wa kirusi hicho.
Dharura ya upimaji inaongezeka wakati maafisa wa afya wanaripoti kuwepo kwa maambukizo mapya ya kirusi cha corona nchini Marekani.
Pia umuhimu wa upimaji ni kutokana na kutokea kwa kifo cha kwanza nchini kutokana na kirusi hicho – mtu mwenye umri wa miaka 50 kutoka jimbo la Washington.
Sera hiyo mpya imezinduliwa Jumamosi na Uongozi unaosimamia chakula na madawa Marekani (FDA), kufuatia malalamiko dhidi ya serikali kuwa ukosekanaji wa vifaa vya kupimia umeruhusu kirusi hicho kuenea bila ya kujulikana.
“Hatua hii kwa kweli itakuwa na tija kwa kuongezwa idadi ya vituo ambavyo vitaweza kupima maambukizi ya kirusi hiki,” alisema Jennifer Nuzzo, msomi wa ngazi ya juu katika kituo cha usalama wa afya chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Hospitali zote zimekuwa zikituma sampuli za vipimo zifanyiwe uchunguzi katika Vituovya Kudihibiti na Kukinga kuenea kwa Maradhi vya Marekani huko Atlanta. Kupata majibu inachukuwa masaa 48.