Malaysia tayari ina maambukizi yaliyo thibitishwa ya wagonjwa 500 na itaweka katazo kwa kiwango fulani kwa kipindi cha wiki mbili.
Nchini Saudi Arabia, maafisa Jumatano wamewaambia wafanyabiashara katika sekta binafsi ikiwezekana kuhakikisha wafanyakazi wao wanatekeleza majukumu yao wakiwa nyumbani, na kwa wale ambao lazima wawepo katika maeneo yao ya kazi kuchukua hatua za kuhakikisha wafanyakazi hawakaribiani.
Australia
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison ametangaza “ hali ya dharura ya kuwalinda binadamu na maambukizi” Jumatano, ikipitisha ruhsa kwa serikali kutangaza katazo la kutoka nje na karantini.
Nchi nyingine tayari zimechukua hatua hizo kusitisha watu kuwa na harakati za kawaida za maisha.
Itali, Hispania, na Ufaransa
Itali, Hispania na Ufaransa hivi sasa zimeweka katazo imara dhidi ya watu kuzunguka majiani wakati wakikabiliana na idadi ya juu ya maambukizi ukilinganisha na nchi nyingine duniani.
Huko Brazil, ambapo tayari kuna maambukizi ya wagonjwa zaidi ya 300, mamlaka inayoangalia mabustani imetangaza kufungwa kwa maeneo hayo kwa mujibu wa muongozo wa afya uliotolewa rasmi ukiwataka watu kuepuka misongamano. Katazo hilo linajumuisha sehemu maarufu ya sanamu la Christo ambalo liko mkabala na eneo la Rio de Janeiro.
Brazil
Brazil ilitangaza kifo cha kwanza cha mtu aliyeambukizwa kirusi cha corona Jumanne.
Virusi vya corona tayari vimewasili katika nchi 159, ambapo maambukizi yaliyopimwa yamefikia 185,000 na vifo ni 7,500, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kyrgyzstan
Kyrgyzstan hivi karibuni imetangaza maambukizo ya kwanza Jumatano. Tayari ilikuwa imeshafunga mipaka yake kwa wageni kuingia nchini humo.