Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:59

IMF yasema kuenea kwa kirusi cha corona kunaweza kudumaza uchumi wa dunia


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)

Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, linasema kwamba kuenea kwa kasi kwa virusi vya corona kutaondoa matumaini yeyote ya ukuaji mkubwa wa uchumi mwaka 2020.

Kauli hiyo imekuja baada ya karibu theluthi moja ya nchi wanachama 189 wa shirika hilo kuathirika tayari na ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo.

Mkurungenzi Mtendaji wa IMF, Kristalina Georgieva, alitoa taarifa hiyo baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati ya utendaji ya IMF.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara

Kwa upande wake mkurugenzi wa kitengo cha biashara ya kimataifa katika shirika la bishara la umoja wa mataifa UNCTAD, Bi Pamela Coke-Hamilton anasema bidhaa muhimu zinazosafirishwa nje na Uchina ikiwa ni pamoja na vipuri vya bidhaa kuanzia magari hadi simu za mkononi zinakadiriwa kushuka kwa asili mia mbili mnemo mwezi wa Februari na hivyo kugharimu mataifa na viwanda vyao karibu dola bilioni 50.

China ambayo ndio kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona huzalisha karibu asilimia 20 ya bidhaa zinazo hitajika kote duniani.

Kudorora kwa uchumi

Shirika hilo la fedha sasa linatarajia uchumi wa dunia kukua kwa kiwango kilicho chini ya asilimia 2. 9 mwaka huu. Takwimu mpya za marekebisho ya ukuaji wa uchumi wa dunia zitatolewa wiki zijazo. Ripoti kamili na Patrick Nduwimana.

Ukuwaji wa uchumi utashuka kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 0.4 kutoka ukuaji wa asilimia 3.3 uliotabiriwa mwezi Januari na IMF, kwa kuzingatia afueni iliyopatikana kwenye mzozo wa biashara kati ya Marekani na China.

Hata hivyo ukuaji wa uchumi mwaka 2020 utashuka ukilinganisha na kiwango cha mwaka uliopita, amesema Georgieva. Lakini amejizuia kusema kwamba kuenea kwa haraka kwa virus vya corona kunaweza kusababisha uchumi wa dunia kudorora

Mfumo wa fedha

Kristalina, mkurugenzi mtendaji wa IMF anaeleza :“Tunajua pia kuwa tuna mfumo mzuri wa kifedha wenye nguvu zaidi kuliko ilivyokua kabla ya mzozo wa kifedha.

Ameongoza : "Hata hivyo, tunakabiliwa na hali isiokua na uhakika ambayo imetulazimisha kutoa utabiri mwengine, utabiri uliotupelekea kusema kwamba ukuaji wa uchumi wa dunia mwaka wa 2020 utashuka ukulinganisha na viwango vya mwaka jana. Lakini ni kwa kiwango gani utashuka au hadi lini, pamoja na athari zake, hilo ni vigumu kulitabiri. Itategemea na janga lenyewe itategemea pia na wakati na ufanisi wa hatua zetu.”

Benki ya Dunia

Georgieva na rais wa Benki ya Dunia David Malpass wamesisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano katika kuchukua hatua ili kudhibiti athari za kiuchumi na kibinadamu zinazotokana na kirusi cha corona.

Kwa upande wake David Malpass, Mkuu wa Benki ya Dunia : “Kuna haja ya kufadhili biashara ndogo ndogo na ubunifu na hilo kufanywa kupitia ufadhili wa kiwango cha chini cha mtaji, na hivyo ndivyo vyombo vinatumiwa na benki ya dunia katika swala hili.

Ni muhimu vichocheo vya kifedha visichukuliwe kutoka kwa rasilimali za mtaji wa kufanya kazi.”

IMF imetenga mfuko wa dharura wa dola billioni 50 kwa nchi wanachama ikiwemo mikopo ya riba ilio chini itakayosaidia nchi maskini kukabiliana na janga hili.

Mlipuko hautabiriki

Georgieva anasema wakati huu ni vigumu kutabiri muda gani mlipuko utadumu, akiongeza kuwa ufanisi na hatua za kudhibiti mlipuko vitakua na fasi muhimu kwa kubaini athari za uchumi.

Georgieva Kristalina, mkurugenzi mtendaji wa IMF anaeleza : “ Hili sio tena tatizo la kikanda. Ni tatizo la dunia nzima ambalo linahitaji jawabu kutoka dunia nzima. Tunajua kwamba mlipuko utakwisha siku moja, lakini hatujuwi lini hili litatokea. Hatujuwi bado virusi vitajibuaje, lini tiba na chanjo vitapatikana.”

Wiki mbili zilizopita, IMF ilisema virusi vitapunguza asilimia 0.1 kwenye utabiri wa ukuaji wa uchumi wa dunia wa mwezi Januari.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Patrick Nduwimana, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG