Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:57

Mlipuko wa virusi vya corona yasababisha Afrika kupoteza dola za Marekani bilioni 29


Nchi za Afrika hadi sasa zimepoteza takriban dola za Marekani bilioni 29 kutokana na mlipuko wa virusi vya corona uliovuruga uchumi wake, kiwango sawa na kipato cha ndani (GDP) cha taifa la Uganda kwa mujibu wa makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Kamisheni ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika katika ripoti yake ya hivi karibuni ilitabiri kuwa mlipuko wa virusi vya corona utaifanya Africa kupoteza asilimia 1.4 ya pato lake la taifa, GDP, la dola trilioni 2.1, kutokana na kusimama kwa biashara kote barani humo na sehemu mbalimbali za dunia.

Ripoti ya UN

Ripoti hiyo inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa mwaka mzima wa bara hilo unaweza kudondoka kutoka asilimia 3.2 mwezi Februari kufikia asilimia 1.8 mwezi Machi, ukitahadharisha kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi katika miezi ijayo wakati nchi nyingi zaidi zinaripoti maambukizi ya virusi vya corona katika nchi zao.

“Afrika inaweza kupoteza nusu ya pato lake la taifa kwa kuanguka kwa ukuaji wa uchumi kwa sababu kadhaa ikiwemo kusambaratika kwa mifumo ya usambazaji bidhaa ya kimataifa,” amesema Katibu Mtendaji wa ECA, Vera Songwe, katika tamko lake.

Kwa mujibu wa gazeti la “The East African,” Uganda’s ato la Taifa la Uganda lilikadiriwa kukua kwa takriban dola bilioni 28.5 ifikapo mwisho wa mwaka 2019, ikionyesha kuwa kadirio la hasara hadi sasa ni sawa na uzalishaji wa mwaka mzima wa nchi hiyo.

Nchi 36 kati ya 54 za Afrika zimethibitisha zaidi ya maambukizo 700 ya virusi vya corona, wakati duniani kote zaidi ya watu 200,000 wameambukizwa na virusi vya Covid -19, na kupelekea vifo 9,000 hadi Ijumaa wiki iliopita, Machi 20.

Katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya, Tanzania na Rwanda zote zimeripoti maambukizi ya virusi vya corona, wakati Uganda, Burundi na Afrika Kusini hazijawasilisha takwimu zozote hadi Ijumaa iliyopita.

Kuzorota kwa ukuaji wa uchumi

Shirika la UN limetahadharisha kuwa kuendelea kwa janga la mlipuka wa virusi vya corona kunaweza kuathiri uchumi wa Afrika ambao tayari umedorora, ambapo bara hilo linatarajia kutumia zaidi ya dola bilioni 10.6 katika kuongezeka kwa ghafla bajeti za afya za nchi hizo ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Dkt Songwe katika tamko lake anaeleza kuwa China, ambayo ni mshiriki mkuu wa kibiashara wa Afrika ambayo imeathiriwa vibaya na virusi vya Covid-19, tayari inaathari hasi kwa biashara ya Afrika kwa kuathiri mifumo ya usambazaji wa mali ghafi na bidhaa duniani.

XS
SM
MD
LG