Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:15

Viongozi wa Marekani wafikia makubaliano ya msaada wa dola trilioni 2


Jengo la Bunge la Marekani.
Jengo la Bunge la Marekani.

Viongozi wa Marekani mapema Jumatano wamesema wamefikia makubaliano ya dola trilioni 2 kuokoa uchumi zitakazotumika kuwasaidia wafanyakazi na biashara kuhimili athari zinazotokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Maudhui ya muswada huo yatatolewa Jumatano asubuhi na kufuatiwa na kura katika Baraza la Seneti. Iwapo Seneti itapitisha, utapelekwa katika Baraza la Wawakilishi.

Kiongozi wa waliowachace katika Seneti Chuck Schumer amesema muswada huo “bado unamapungufu,” lakini baada ya kufanya maboresho katika masiku ya majadiliano ni lazima upitishwe kwa haraka.

“Tumefikia makubaliano ya pande mbili katika kiwango kikubwa zaidi cha fedha zitakazo okoa uchumi katika historia ya Marekani,” Schumer amesema. “Huu siyo wakati wa kusheherekea, lakini ni moja ya mahitaji muhimu.”

“Msaada uko njiani,” Kiongozi wa waliowengi Mitch McConnell amesema.

Ameeleza hatua hiyo ya kuokoa uchumi kuwa nia habari njema kwa madaktari na wauguzi nchini ambao wanahitaji fedha zaidi na vifaa vya kujikinga na maambukizi wakiwa kazini kama vile maski wakati wakiwahudumia wagonjwa wenye virusi.

Pia amesema ni faraja pia kwa familia mbalimbali ambao watapatiwa malipo ikiwa ni sehemu ya juhudi za “kuingiza trilioni” za dola katika uchumi wa Marekani. “Kwa kweli, uwekezaji huu ni wa kiwango cha wakati wa hali ya vita kwa taifa letu,” amesema Mc Connell.

Rais Donald Trump anasema anataka uchumi wa Marekani uanze kufanya kazi kwa haraka iwezekanavyo wakati amri ya kujizuilia majumbani ikiwa inatekelezwa na majimbo mengi ya Marekani ambapo wafanyakazi wako majumbani na biashara kama vile migahawa, mabaa na majumba ya sinema yamefungwa.

Msaada huo wa fedha unalenga kuboresha uchumi wa Marekani kwa kutuma malipo moja kwa moja kwa zaidi ya asilimia 90 ya Wamarekani na biashara mbalimbali za Marekani kuwasaidia mara moja kuhimili kuongezeka kwa athari za uchumi zinazotokana na maambukizi ya virusi vya corona.

XS
SM
MD
LG