Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:02

Serikali za Afrika zachukuwa hatua kali kupambana na maambukizi ya virusi vya corona


Takriban serikali zote za Afrika zimetangaza hatua kali za kupambana na janga hilo la afya ambalo halijawahi kushuhudiwa kote duniani, ambapo mataifa yamefunga mipaka yake, kuahirisha safari za ndege na kupitisha hatua kali za karantin.

Vyanzo mbalimbali vya habari vinaeleza kuwa janga hilo la corona ambalo hakuna aliyetazamia hivi sasa limeathiri zaidi ya nusu za nchi za Afrika.

Kumeripotiwa idadi ndogo sana ya watu walioambukizwa na virusi vya corona barani humo, na kulisababisha Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhoji hii leo ikiwa idadi ya watu waloambukizwa ni sahihi.

Ripoti ya WHO

Hadi kufikia Jumatano wiki hii WHO imepokea ripoti za watu 233 waloambukizwa na watu 4 wamefariki kutokana na janga hilo ikiwa idadi ya chini kabisa kati ya kanda zote za dunia.

Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dk Tedros Ghebreyesus , anasema tofauti kubwa kati ya idadi ya waloambukizwa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na maeneo mengine ya dunia huenda ikawa ni ishara ya utaratibu dhaifu wa afya na upungufu wa vifaa vya kupima katika baadhi ya nchi.

Amesema hajaweza kukubaliana na takwimu hizo namna zilivyo huenda kuna watu wengi zaidi hawajatambulika bado.

Ghebreyesus anasema wanadhani idadi ya watu 233 ni ndogo kwa vile katika maeneo mengine ugonjwa unaoendelea maambukizaji yanasambaa kwa kasi kabisa ndio maana wanajiuliza inakuwaje idadi ni ndogo hivyo.

Mataifa ya Afrika

Anasema mataifa ya Afrika yanabidi kujitayarisha kwa kuwa na utaratibu bora wa kupima na kuwaweka watu katika karanti ili kuepusha uwezekano wa kuenea zaidi.

Idadi hiyo ndogo imezusha dhana kote Afrika kama Waafrika hawaambukizwi na virusi hivyo lakini hadi hivi sasa hakuna uchunguzi wa kisayansi kuthibitisha dhana hiyo.

Kulingana na takwimu za mashirika mengine idadi ya waloambukizwa Afrika imefikia 627 na watu 40 wamefariki. Na maafisa wa WHO wanatahadhariusha juu ya kusamba kwa habari za uwongo juu ya ugonjwa huo na kuzitaka serikali kuhakikisha watu wanaelimishwa juu ya hatari.

Africa

Hata hivyo mkurugenzi kwa ajili ya Afrika Rebecca Moeti aliwambia waandishi habari mapema wiki hii kwamba uwezo wa nchi za Afrika kukabiliana na janga hilo umeanza kuimarika tangu kutangazwa mtu wa kwanza aliyeambukizwa na ugnjwa huo nchini Misri.

Nchi za Afrika kaskazini ndio zina idadi kubwa ya watu waloambukizwa barani humo.

Katika kusaidia nchi za Afrika China imeshaanza kupeleka maelfu ya vifaa vya kupima ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona na wanatarajia zaidi wiki ijayo kulingana na mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa cha Afrika John Nkengasong.

Vifaa vilivyopokelewa

Anasema hadi hivi sasa wamepokea vifaa 2000 kutoka china na wameshasambaza kwa baadhi ya mataifa na wanataraji kupokea vifaaelfu 10 wiki ijayo.

Unkengasong anasema huenda bara hilo likashuhudia idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa mnamo wiki zijazo kwa sababu kuna watu waloambukizwa kutoka nje huwenda wameingia bila kugundulikana. Hadi hivi sasa katika takriba maaifa yote ya afrika watu waloambukizwa ni ageni na wahamiaji wa afrika wanaotokea nje.

Afisa wa juu barani Afrika kufariki kutokana na ugonjwa wa corona ni Makamu Rais wa kwanza wa bunge la Burkina Faso Rose Marie Compaore aliyekua na umnri wa miaka 62, na anaripotiwa alikua na kisukari.

XS
SM
MD
LG