Waziri wa Afya Zweli Mkhize amethibitisha vifo hivyo, akisema marehemu wote hao walifia Magharibi mwa Cape province
Afrika Kusini ina zaidi ya watu 1,000 walioambukizwa virusi hivyo, ikiwa idadi kubwa zaidi katika Afrika, ambapo zaidi ya watu 3,000 barani humo wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa virusi vya corona.
Amri ya kukaa majumbani iliyotangazwa Afrika Kusini, ambayo imeanza kutekelezwa Ijumaa, inachukuliwa kwa makini sana, wakati uuzaji wa pombe na watu kuwatembeza mbwa wao barabarani kukatazwa kati ya mambo mengine.
Watu pia wamekatazwa kukimbia mitaani kwa kipindi cha wiki tatu zijazo. Lakini wanaruhusiwa kutoka nje to kwenda kutafuta mahitaji muhimu ikiwemo matibabu na chakula.
Mipaka ya Afrika Kusini tayari imeshafungwa na watu hawaruhusiwi kuingia nchini humo, lakini bidhaa muhimu zinaweza kuingia nchini.
Katazo la kutotoka majumbani linaweza kuendelea kwa siku 21 iwapo hali ya maambukizi ya virusi vya corona haitabadilika.