Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:06

Wakati idadi ya vifo Marekani ikipindukia 5,000, Meya wa Los Angeles ahimiza watu kuvaa maski


Huyu ni Meya wa Jiji la Los Angeles Eric Garceti akihamasisha watu kuvaa maski kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa kila siku Los Angeles, Jumatano Aprili 1, 2020.(Office of Mayor Eric Garcetti via AP)
Huyu ni Meya wa Jiji la Los Angeles Eric Garceti akihamasisha watu kuvaa maski kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa kila siku Los Angeles, Jumatano Aprili 1, 2020.(Office of Mayor Eric Garcetti via AP)

Wakati idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona ikiwa imepindukia watu 5,000 Marekani, Meya wa Jiji la Los Angeles amewataka watu katika mji wa pili kwa ukubwa nchinikuvaa maski wanapokuwa katika maeneo ya umma.

Meya Eric Garcetti amesema watu wasitumie maski ambazo ni za huduma za tiba ambazo ni haba sokoni na zinahitajika sana na wahudumu wa afya, lakini amesema kutumia maski zilizotengenezwa kwa vitambaa itapunguza maambukizi ya virusi hivyo.

Maafisa wa afya wa serikali kuu hadi sasa hawajashauri watu wavae maski.

Garcetti pia amesema kuvaa maski sio ruhusa ya kuwafanya watu “waanze wote kutoka nje,” na kwamba ni lazima waendelee kukaa majumbani isipokuwa pale wanapohitajika kutekeleza majukumu muhimu kama vile kununua chakula.

Idadi ya maambukizi yanakaribia kufikia watu milioni 1 duniani na vifo 50,000. Hadi Alhamisi idadi ya vifo duniani kutokana na virusi vya corona imefikia 1,098 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa na vifo vipya viwili katika idadi hiyo.

Afrika

Wakati huohuo Mataifa ya Afrika yanaendelea kutangaza mbinu kali za kudhibithi maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimeua zaidi ya watu 200 barani humo.

WHO

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa haraka kwa maambukizi hayo.

Pia amegusia shinikizo wanalokutana nalo watu maskini na watu ambao maisha yao yako hatarini katika maeneo ambayo kuna amri ya kukaa majumbani na ameomba nchi zinazoendelea zisaidiwe iwapo hazina rasilmali kuweza kupanua programu zao za huduma za mahitaji ya kijamii.

CDC

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimeonya Jumatano kuwa mtu yoyote anaweza kubeba virusi vya corona hata kama hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa huo.

CDC imethibitisha tafiti kutoka Singapore inayosema kuwa asilimia 10 ya maambukizi mapya yanasambazwa na watu ambao hawana dalili zozote za kuwa wagonjwa. Tafiti hiyo ina thibitisha haja ya kuendelea watu kutosongamana na kutokaribiana, CDC imesema.

Boris Johnson

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye amejitenga baada ya kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, amesema katika ujumbe wake kwa njia ya video kuwa Uingereza “itaongeza upimaji wa wananchi” wake ikiwa ni hatua ya msingi ya hatimaye kutokomeza virusi hivyo.

Itali

Itali ni imeathiriwa vibaya sana kuliko nchi nyingine kwa kiwango cha vifo, ikiwa na zaidi ya vifo 13,000. Viongozi wake wametangaza Jumatano kuendeleza amri ya watu kutotoka nje ya nyumba zao kwa matumaini ya kuendelea kuwepo maambukizi machache zaidi ikiwa ni hatua ya kudhibiti mlipuko wa maradhi haya nchini humo.

Hispania

Hispania, ambayo pia inaendeleza amri ya kutotoka nje kwa wiki kadhaa baada ya kuenea kwa haraka wa virusi vya corona, imetangaza Alhamisi kuwa kiwango cha vifo kimezidi watu 10,000, ikifanya nchi hiyo kuwa ya pili duniani kupita kiwango hicho.

Ubelgiji

Ubelgiji ina idadi kubwa ya maambukizi ukilinganisha na ukubwa wa nchi hiyo, ikiripoti Alhamisi imethibitisha watu 15,000 wameambukizwa virusi hivyo, na hivyo vifo ni zaidi ya 1,000. Ikiwa na idadi ya watu milioni 11.4, Ubeljiji ina karibia kuwa katika nchi 10 duniani kwa idadi zote mbili.

Mexico

Huko Mexico, wizara ya mambo ya nje amewashauri wananchi wa Mexico wanaoishi katika nchi – hasa Marekani – wasisafiri kuja nyumbani kutembelea familia zao hivi sasa kwa sababu ya hatari ya kuleta maradhi hayo.

Israeli

Wizara ya afya ya Israeli imetangaza Alhamisi kuwa kiongozi wake,Yaakov Litzman, ameabukizwa virusi vya corona na hivi sasa amejitenga.

Burundi

Serikali ya Burundi imezuia magari ya mizigo kutoka Kenyana Uganda, yanayopitia Rwanda kuingia nchini mwake, licha ya makubaliano baina ya nchi hizo kuendelea kuruhusu usafiri wa mizigo.

Afrika Kusini

Waziri wa Afya wa Afrika kusini Dkt Zweli Mkhize, ameeleza wasiwasi kuhusiana na ongezeko la maambukizi ndani ya nchi.Serikali ya Afrika kusini imeanzisha hatua ya kupima watu kutoka mlango hadi mlango.

Maabara ya kitaifa imetuma maafisa wake katika sehemu zote za nchi hiyo wakiwa na vifaa maalum vyenye uwezo wa kuwapima watu 5,000 kila siku.

Wakati huo huo, serikali ya Afrika kusini imeruhusu magari ya kubeba abiria, kubeba watu kadhaa ilimradi wamejifunika midomo na pua ili kuzuia maambukizi.Wahudumu wa magari walikuwa wametishia kufanya mgomo kufuatia amri ya kudhibithi idadi ya wateja wanaostahili kubeba.

Kenya

Nchini Kenya, idadi ya maambukizi imeongezeka zaidi, huku baadhi ya watu waliokuwa wamelazwa, wakiruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupona.

Uganda

Nchini Uganda, hali ya afya ya wanakwaya tisawakiwemo Watoto, walioambukizwa Corona, inaendelea kuimarika.Kundi hilo liligunduliwa kuambukizwa baada ya kumaliza siku 14 za kutengwa.Walikuwa wamesafiri Marekani, Canada na Uingereza.

Rwanda

Serikali ya Rwanda imeongeza mda wa kusitisha shughuli za kawaida nchini humo hadi April 19. Mipaka yake itaendelea kufungwa.Amri hiyo ya Rwanda ilianza march 21. Watu hawaruhusiwi kuondoka nyumbani kwao kando na kwenda dukani kununua chakula au dawa. Polisi wameshika doria kuhakikisha kwamba amri hiyo inaheshimiwa.

Kenya

Kenya itapokea dola milioni 50 kutoka kwa benki kuu kusaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.Waziri wa afya Mutahi Kagwe, amesema pesa hizo zitatumika kununua vifaa vya afya hasa vya kuwakinga wafanyakazi wa afya dhidi ya maambukizi, kufanya utakasaji na kuongeza idadi ya vitanda kwa wagonjwa hispitalini.

XS
SM
MD
LG