Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:55

Nchi zaidi zaendeleza masharti ya watu kutotoka nje kukabiliana na virusi vya corona


Watu wa Dayosisi ya Kanisa la Amritsar Kaskazini mwa India wakigawa maski kwa wananchi wakati serikali ya India ilipotangaza amri ya kutotoka nje kudhibiti janga la corona Aprili 15, 2020. (Photo by NARINDER…
Watu wa Dayosisi ya Kanisa la Amritsar Kaskazini mwa India wakigawa maski kwa wananchi wakati serikali ya India ilipotangaza amri ya kutotoka nje kudhibiti janga la corona Aprili 15, 2020. (Photo by NARINDER…

Mataifa mengi ya dunia hasa Ulaya yameongeza muda wa watu kubaki nyumbani wakati idadi ya maambukizi ikiongezeka huku baadhi yakianza kupunguza masharti ya kutotoka nje. 

Kulingana na takwimu za chuo kikuu cha John Hopkins hapa Marekani watu 2,206,348 walioambukizwa kufikia Ijumaa na zaidi ya watu 148,649 waliofariki.

Wakati hali ya janga hili ikiendelea watu wengi zaidi wanazidi kupoteza ajira na kusababisha baadhi ya mataifa kutangaza misaada mikubwa ya kifedha kujaribu kuokoa uchumi.

Siku ya Alhamisi, Canada na Misri zimetangaza msaada wa dharura wa mamilioni ya dola na India kupunguza kiwango cha riba ili kuokoa uchumi wake.

Uingereza Mexico na Ureno zimetangaza muda zaidi wa watu kubaki majumbani.

Wakati huohuo Shirika la Afya Duniani WHO linazihimiza serikali za Afrika na Mashaiki ya Kati kuchukuwa nafasi hii ya kupambana na janga la Corona kuimarisha mifumo yao ya afya wakati idadi ya maabukizi ya virusi vya corona ingali ndogo ukilinganisha na maeneo mengine ya dunia.

Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya kuambukiza katika Ofisi ya WHO, kanda ya Mashariki ya Kati Yvan Hutin, ameliambia shirika la habari la AFP mjini Cairo kwamba inabidi serikali za kanda hizo kuchukuwa hatua za haraka hivi sasa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mambukizi ingawa ni ndogo.

Amezitaka nchi hizo kendelea kuimarisha huduma za afya, hospitali, juhudi za kuwahamasisha wananchi na kuongeza uwezo wa kuwapima watu.

Katika kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika kuna watu 110,000 walioambukizwa na zaidi ya watu 5,500 waliofariki. Iran ndio nchi iliyoathirika zaidi katika kanda hiyo ikiwa na watu 78,000 walioambukizwa na 5,000 waliofariki.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG