Hii ni kufuatia wito uliotolewa na askofu wa Pemba Luis Fernado Lisboa, kutaka msaada kwa maelfu ya watu waliofurushwa makwao na wavamizi wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.
Wanamgambo hao wamekuwa wakifanya mashambulizi katika eneo hilo tangu mwaka wa 2017 na takriban watu 430,000 wamebaki bila makazi.
Askofu Liboa aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba msaada huo, utatumiwa kujenga vitoa vya afya, hususan katika maeneo ambako wakimbizi wengi wanahifadhiwa, katika wilaya za Montepuez na Chiure.