Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:22

Msumbiji yapata mamilioni ya dola kutoka EU kukabiliana na Covid


Umoja wa ulaya umekubali kutoa dola milioni 116 kwa serikali ya Msumbiji kusaidia kupambana na janga la virusi vya Corona.

Umoja huo ulipunguza msaada wake wa kifedha kwa msumbiji mnamo mwaka 2016 baada ya nchi hiyo kufichua taarifa za kuwa na madeni mengi kutokana na mkopo, yaliyokuwa yamesimamiwa na serikali.

Serikali ilikuwa imeficha taarifa kuhusu mikopo hiyo.

Wafadhili wengine ikiwemo shirika la fedha la kimataifa IMF, walisitisha msaada wao kwa Msumbiji.

Balozi wa umoja wa ulaya Antonio Sanchez-Benedito Gaspar ameambia waandishi wa habari mjini Maputo kwamba msaada huo utatumika moja kwa moja kusaidia watu wa Msumbiji kukabiliana na athari za kiuchumi kutokana na janga la virusi vya Corona.

Kufikia sasa, watu 13, 130 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Msumbiji, 94 wamefariki dunia.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG