Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:20

Sirro akiri Watanzania kuhusika na kundi la uhalifu mpakani Msumbiji


FILE -Mabaki ya makazi yaliyochomwa moto katika kijiji cha Aldeia da Paz nje kidogo ya mji wa Macomia, katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini ya Msumbiji, Aug. 24, 2019.
FILE -Mabaki ya makazi yaliyochomwa moto katika kijiji cha Aldeia da Paz nje kidogo ya mji wa Macomia, katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini ya Msumbiji, Aug. 24, 2019.

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania Simon Sirro amekiri kuna Watanzania wanahusika katika kundi la kihalifu linalofanya mauaji, utekaji na uchomaji wa nyumba mpakani mwa Msumbiji na Tanzania, wakitokea nchini Msumbiji.

Katika Mkutano wake na waandishi wa habari Alhamisi jijini Dar es Salaam Mkuu wa jeshi la polisi, IGP, Sirro amesema kwamba katika eneo la Kitaya mkoani Mtwara ambako kundi hilo lilivamia, kumekuwa na matukio ambayo yanadhihirisha kuwa kuna watanzania wanahusika na kundi hilo la kihalifu kutoka nchini Msumbiji.

Licha ya kuwataka wakazi wa maeneo ya mpakani na Msumbiji kuendelea na shughuli zao kwa vile hali ya usalama kwa sasa imeimarishwa , Sirro bado ametahadharisha vijana wa kitanzania ambao amesema wanao ushahidi na wao kujiingiza katika kundi hilo la kihalifu nchini Msumbiji kutoka mikoa mbalimbali nchini

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Jeshi la Polisi ametoa tathmini ya hali ya nchi baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Octoba 27 na 28 Tanzania bara na visiwani ambapo ameeleza kushangazwa na madai ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao wameleeza kutishiwa maisha na hata kulazimika kutafuta hifadhi nje ya nchi.

Hata hivyo IGP amesema kwamba jeshi la polisi kwa sasa linawashikilia watu takribani 254 kati ya mahabusu mbalimbali nchini baada ya kudaiwa kujihusisha na vurugu za wakati wa Uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG