Maelfu ya watu wanahofiwa kukimbia makazi yao kufuatia mashambulizi mabaya ya kundi linalohisiana na Islamic State katika mji wa uzalishaji wa gesi uliopo kaskazini mwa Msumbiji.
Shirika la habri la Reuters linaripoti kwamba waokozi walikuwa wakitafuta walionusurika huku wengi wao wakiaminika kukimbia katika misitu ama wakijaribu kukimbia kwa kutumia maboti baada ya mji wa Palma kushambuliwa Jumatano kwa mujibu wa wafanyakazi wa misaada waliozungumza na Reuters.
Serekali ya Msumbiji imethibitisha kutokea kwa dazeni ya vifo, ikijumuisha watu saba ambao waliuwawa baada ya wanamgambo kuvamia msafara wa magari ukijaribu kutoroka hoteli ambayo ilikuwa imehifadhi baadhi ya watu.
Mashuhuda wameeleza kuwa maiti zilizagaa mitaani huku baadhi yao zikiwa zimechinjwa.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu mausla ya kibinadamu (OCHA) imesema kwamba iliendelea kupokea ripoti za mapigano ya Palma, na maeneo ya jirani kwa siku ya Jumanne.