Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:00

Watoto 125 wakamatwa Libya wakisafirishwa kwenda Ulaya


Ramani ya Libya
Ramani ya Libya

Jumla ya watoto 125 waliokuwa wanasafirishwa kwenda Ulaya ni kati ya wale waliokamatwa baharini wiki hii na mamlaka ya Libya nje ya pwani ya bahari ya Mediterranean, shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia maslahi ya watoto limesema Ijumaa, likiongeza kuwa wengi wanashikiliwa katika vituo kadhaa.

Watoto ambao wanakimbia vita na umaskini hutumia usafiri hatari wa baharini kuelekea Ulaya, ulijumuisha watoto 114 waliosafiri peke yao, UNICEF imeongeza katika taarifa yake.

“Wengi wa wale waliookolewa wanapelekwa katika vituo vya kuwashikilia ambavyo vina msongamano nchini Libya vyenye hali mbaya kabisa na bila au kiasi kidogo cha upatikanaji wa maji na huduma za afya. Takriban watoto 1,100 wako katika vituo hivi,” imeeleza taarifa hiyo.

UNICEF imeisihi mamlaka nchini Libya kuwaachia watoto wote na kuacha kuwashikilia katika vituo vya uhamiaji.

Katika miaka hiyo tangu maandamano yaliyokuwa yanaungwa mkono na NATO 2011 yaliopelekea kupinduliwa na kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi, Libya iliyoko katika vita imekuwa ni sehemu kuu ya kituo cha mpito cha wahamiaji wanaokimbia Afrika na Mashariki ya Kati.

XS
SM
MD
LG