Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:49

Marekani yafungua mashitaka dhidi ya mshukiwa wa shambulizi la PanAm


Mashada ya maua katike eneo la kumbu kumbu ya waathirika wea shambulizi la ndege ya PanAm karibu na Lockerbie Scotland.
Mashada ya maua katike eneo la kumbu kumbu ya waathirika wea shambulizi la ndege ya PanAm karibu na Lockerbie Scotland.

Wizara ya Sheria ya Marekani imetangaza mashtaka dhidi ya afisa mmoja wa zamani wa ujasusi wa Libya ambaye anadaiwa kutengeneza bomu lililolipuka ndani ya ndege ya Pan Am nambari 103 juu ya anga la Lockerbie, Scotland miaka 32 iliyopita.

Jumatatu Desemba 21, 2020 yalikuwa ni maadhimisho ya miaka 32 ya mlipuko huo wa mwaka 1988, ambao uliangusha ndege hiyo kwenye anga ya Lockerbie na kuuwa watu wapatao 270. Mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr aliwaamba waandishi wa habari, akielezea imani kwamba ataletwa Marekani kwa ajili ya kesi hiyo Marekani.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr anasema serikali ya nchi hiyo ina matumaini kwamba raia huyo wa Libya ambaye alishtakiwa katika shambulizi la bomu la ndege ya Pan Am nambari 103 mnamo mwaka 1988 atakabidhiwa kwa mamlaka nchini Libya.

Barr alitangaza mashtaka yanayohusiana na ugaidi dhidi ya Abu Agila Muhammad Mas'ud Kheir Al-Marimi kwa shutuma ya kushiriki kwake katika shambulizi lililouwa watu 259 ndani ya ndege na watu wengine 11 ardhini.

“Tunadhani matarajio ni mazuri sana. Masud yuko chini ya ulinzi wa serikali ya sasa ya Libya na hatuna sababu ya kufikiria serikali hiyo inavutiwa kujihusisha na kitendo hiki kibaya cha ugaidi, na hivyo tuna matumaini kwamba watamkabidhi ili kukabiliana na mkondo wa sheria."alisema Barr.

Wachunguzi wa Marekani na Scotland waliandaa kesi kwa miaka kadhaa dhidi ya Masud, anayedaiwa kuwa mtengenezaji mkuu wa mabomu wa kiongozi wa zamani wa Libya hayati Moamer Gadhafi.

Mwanasheria huyo Mkuu wa Marekani anayemaliza muda wake pia alitoa maoni yake juu ya mashambulizi ya hivi karibuni ya mtandao dhidi ya Marekani na madai yasio na msingi ya Rais Donald Trump juu ya udanganyifu na wizi wa kura.

“Kwa taarifa niliyo nayo, ninakubaliana na tathmini ya waziri Pompeo kwa kweli inaonekana kuwa ni Russia lakini sitaizungumzia zaidi ya hapo.” Barr aliongeza.

Barr agusia uchunguzi wa mtoto wa Biden

Barr pia aligusia pia uchunguzi juu ya ulipaji kodi wa Hunter Biden, mtoto wa Rais Mteule wa Marekani Joe Biden.

“Kwa kiwango ambacho kuna uchunguzi, nadhani kuwa inashughulikiwa kwa uwajibikaji na kwa weledi kwa sasa ndani ya idara. Na hadi sasa sijaona sababu ya kuteua mwendesha mashitaka maalum na sina mpango wa kufanya hivyo kabla ya kuondoka.” Alisema Barr.

Barr anaondoka madarakani wiki ijayo, baada ya Rais Donald Trump kutangaza Jumatatu kwamba amekubali kujiuzulu kwake, baada ya wiki kadhaa za mvutano dhahiri kati ya rais na afisa huyo mkuu wa sheria nchini Marekani.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washigton DC

XS
SM
MD
LG