Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:28

Pompeo ataja mkataba wa kusitisha vita Libya kuwa hatua ya ujasiri


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, ametaja hatua ya kupatikana makubaliano ya kusitisha vita kati ya pande zinazohasimiana nchini Libya kuwa ya ujasiri na kutaka wapiganaji wote wa nje kuondoka nchini humo katika mda wa siku 90 kulingana na masharti ya mkataba huo.

Pompeo, ambaye amewasili New Delhi katika ziara yake ya kwanza ya Asia, amesema kwamba ni muhimu kwa pande zote husika latika mgogoro wa Libya, kuunga mkono mkataba huo wa Geneva, ambao umesimamiwa na umoja wa mataifa.

“Tunapongeza uongozi wa pande zote husika katika mgogoro wa Libya kwa kuchukua hatua hii ya ujasiri,” amesema Pompeo katika taarifa kwa waandishi wa habari.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG