“Inavunja moyo kushuhudia hofu na uvunjifu wa amani unaofanywa na wale waliojichukulia madaraka kwa nguvu huko Myanmar,” ambayo pia inajulikana kama Burma. Thomas Andrews ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la UN Ijumaa.
Akielezea juu ya suala hilo, mkurugenzi wa masuala ya kisekta TCRA, Emanuel Manase, amesema itakuwa vigumu kwa mdhibiti wa mawasiliano kuzuia simu za WhatsApp lakini amegusia kuwa kuboresha mifumo ya udhibiti ya TCRA kutaangazia kuimarisha kipato cha serikali kwa kubuni ushuru mpya wa data.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Papa Francis, amekutana Jumamosi mjini Iraq na Ayatollah Ali al-Sistani, kiongozi wa Kiislamu wa dhehebu la Kishia.
Marekani inaelekea kufikia maambukizi milioni 30, ikifuatiwa na India yenye maambukizi milioni 11 na Brazil milioni 10.8.
Wakristo nchini Iraq wana matumaini maoni ya al-Sistani na ujumbe wa Francis wa watu kuishi kwa kuvumiliana utasaidia kurahisisha maisha yao katika nchi yenye Waislam wengi, ambapo wanajikuta mara nyingi wakishambuliwa na wanamgambo wafuasi wa dhehebu la Shia.
"Hii inaonyesha kuna haja kwa Tanzania kuchukua hatua za haraka kuwalinda watu wake na kuzilinda jamii nyingine katika nchi jirani na ulimwenguni. Hali hii inatia wasiwasi mkubwa. Ninarejea wito wangu kwa Tanzania kuanza kuripoti maambukizi ya COVID-19 na kushirikiana kutoa takwimu,”
Mkataba wa 2015, JCPOA, ulifikiwa kati ya Iran na wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Ujerumani, wanaojulikana kama “P5+1.”
Hatua hiyo imefikiwa katika kikao chake Jumamosi asubuhi ambapo Maseneta Warepublikan watano na Maseneta Wademokrat 50 walikubaliana kuwaita mashahidi. Lakini Maseneta Warepublikan 45 walipinga hatua hiyo.
Goodman aliwaongoza waliokuwa wakifanya ghasia katika eneo mbali na kule walikokuwa wabunge wakati genge la wafuasi wa Trump wakifanya uharibifu ndani ya Jengo la Bunge kipindi ambacho bunge lilikuwa linakutana kurasimisha ushindi wa uchaguzi wa Rais Joe Biden.
Mapinduzi hayo ya kijeshi yamelaaniwa na Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wengine wa dunia, wakitaka serikali iliyochaguliwa na wananchi kurejeshwa madarakani.
Juan Carlos Sikaffy, rais wa Baraza la Biashara Binafsi Honduras, ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Honduras “haiwezi kusubiri mchakato unaofuata urasimu au maamuzi yanayo potoshwa” kuwapatia wananchi “hali ya utulivu” kwa kuwapatia chanjo ya COVID-19.
“Hatuwafuatili watu kwa sababu za mafungamano yao ya kisiasa au Imani zao za kisiasa au matamshi yao au shughuli zao za kisiasa zinazo lindwa na katiba,” ...“Sisi tunafuatilia vitendo vya uvunjifu wa amani.”
Mawakili wawili mashuhuri kutoka jimbo la South Carolina, Butch Bowers na Deborah Barbier, walitarajiwa kuwa ni mawakili viongozi wa Trump. Lakini, taarifa za vyombo vya habari Jumamosi zimesema kumekuwa na makubaliano ya kutomwakilisha Trump katika kesi hiyo.
Timothy P. Blodgett, kaimu askari msimamizi wa bungeni, ameandika katika barua pepe kuwa jeshi la polisi linaweka mawasiliano maalum na wabunge, na pia amewasihi kuripoti vitisho au vitendo vinavyotia shaka, wanaweza kuwafahamisha mipango yao ya kusafiri.
Seneta wa Marekani Bob Menendez wa New Jersey amesema anapanga kushirikiana na utawala wa Rais Joe Biden kuitaka Uganda iwajibike kutokana na dosari hizo za uchaguzi.
... mazungumzo mapana kati ya viongozi hao yaligusia ulimwengu kukabiliana na janga la virusi vya Corona na tangazo la uongozi wa Biden wiki hii kuwa Marekani itajiunga tena na mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris na kuendeleza ushirikiano wake na Shirika la Afya Duniani, WHO.
Pia alitarajiwa kuongea kwa simu na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg na kupewa muhtasari wa taarifa za operesheni zinazoendelea China na Mashariki ya Kati.
Raia wa Tanzania, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar (Burma), Nigeria, Sudan hawahusishwi tena na katazo la visa za uhamiaji zilizo tangazwa Januari 2020 na Trump.
Joe Biden ameapishwa Jumatano kuwa Rais wa 46 wa Marekani pamoja na Makamu Rais Kamala Harris, Seneta wa zamani Baraza la Seneti la Marekani.
Katika hotuba yake ya kuapishwa, Biden amesema “Matakwa ya watu yamesikika, na yamezingatiwa. Tumejifunza mara nyingine kuwa demokrasia ni yenye thamani na demokrasia inaweza kuharibika. Katika saa hii, Rafiki zangu, demokrasia imeshinda.”
Pandisha zaidi