Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:32

Uongozi wa Biden ‘unafuatilia uvunjifu wa amani’ kudhibiti ugaidi wa ndani


Rais Joe Biden, akiwa na Makamu Rais Kamala Harris, wakizungumza na Spika Nancy Pelosi na viongozi wengine White House, Friday, Feb. 5, 2021, in Washington. (AP Photo/Alex Brandon)
Rais Joe Biden, akiwa na Makamu Rais Kamala Harris, wakizungumza na Spika Nancy Pelosi na viongozi wengine White House, Friday, Feb. 5, 2021, in Washington. (AP Photo/Alex Brandon)

White House na maafisa wa Wizara ya Ulinzi wanatetea maamuzi ya kutathmini kwa undani  hatari ambazo vikundi vya siasa kali vya wazungu ndani ya Marekani vinaendeleza, na kupuuzia ukosoaji dhidi ya hatua hiyo kuwa hatua hizo zitapelekea kile wanachokiita mtihani wa kisiasa. 

Ghadhabu za awali juu ya juhudi hizo mpya kuangalia vikundi vya siasa kali ndani ya Marekani kufuatia uvamizi wa Januari 6 ndani ya Jengo la Bunge la Marekani zimeendelea kuongezeka siku za karibuni, kutokana na uamuzi wa Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin kuamuru shughuli za kijeshi kusitishwa ili kuchunguza ukubwa wa tatizo hili.

FILE - Wafuasi wa Rais Donald Trump wakiwashambulia maafisa wa polisi Bungeni baada ya kuvamia Congress, Washington, Jan. 6, 2021.
FILE - Wafuasi wa Rais Donald Trump wakiwashambulia maafisa wa polisi Bungeni baada ya kuvamia Congress, Washington, Jan. 6, 2021.

Uongozi wa Biden ulikataa upingaji huo Ijumaa, ukisisitiza kuwa hakuna ambaye anajaribu kuingilia haki ya kikatiba ya uhuru wa kujielezea.

“Hatuwafuatili watu kwa sababu za mafungamano yao ya kisiasa au Imani zao za kisiasa au matamshi yao au shughuli zao za kisiasa zinazo lindwa na katiba,” afisa mwandamizi amewaambia waandishi jioni Ijumaa kwa sharti jina lake lisitajwe kutokana na suala hilo kuwa nyeti. “Sisi tunafuatilia vitendo vya uvunjifu wa amani.”

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi alikanusha mapema kabisa madai hayo.

“Hoja ya kuwa hatua hii ya kuchunguza vikundi vya siasa kali kwa hakika ni mtihani wa kisiasa, hilo sio kweli na wala halipo kabisa,” Msemaji wa Wizara ya Ulinzi John Kirby alisema wakati akitoa muhtasari huo Ijumaa.

“Tunawasihi wanajeshi wetu kupiga kura. Tunashawishi kujiandikisha na vyama vya saisa wanavyo vipenda,” Kirby ameeleza zaidi.

“Bila ya kujali ni motisha ya namna gani, unapovunja amri nzuri na nidhamu. Unapokiuka kanuni za uadilifu wa kijeshi, unapovunja sheria za kiraia, hapo tuna tatizo.”

Baadhi ya ukosoaji zaidi wa umma uliotolewa umesikika kutoka kwa mbunge mpya mrepublikan aliyechaguliwa Lauren Boebert, kutoka Colorado, aliyetuma ujumbe wa Twitter Alhamisi kwamba kusitisha shughuli zote za Wizara ya Ulinzi “si jingine bali ni jaribio la kisiasa la mashujaa wetu wanaume na wanawake.”

“Ni fedheha na hatari kuwatumia wanajeshi ambao wanahatarisha maisha yao kuilinda Marekani kwa maslahi ya kisiasa,” amesema.

XS
SM
MD
LG