Waasisi wa taifa hili wamewapa marais nguvu kamili za misamaha ili kulainisha ukingo wa sheria za uhalifu zisizopindika, anasema Brian Kalt, mhadhiri wa sheria chuo kikuu cha Michigan kitengo cha sheria.
“Waliijadili na kuamua kuwa madaraka yanaweza kutumika vibaya, lakini ilikuwa muhimu wawe na uwezo wa kusamehe, hata kwa uhaini, kwa sababu kama [Alexander] Hamilton alivyojadili katika Nyaraka za Wafederali, kunaweza kuwa na uasi unaendelea, na inaweza kuwa njia nzuri yakumaliza uasi huo.”
Hiyo ndio ilikuwa tukio lililojiri na msamaha wa kwanza uliotolewa na George Washington Novemba 2, 1795.
Rais wa kwanza wa Marekani aliwasamehe watu wawili waliokuwa wamehukumiwa kifo kutokana na uasi ambao ulijulikana kama Uasi wa Whiskey.
Watu hao walikuwa ni sehemu ya mgomo wa wazalishaji pombe wakipinga kodi kubwa zilizo wekwa katika bidhaa za ulevi. “Na hivyo, katika hali hiyo ilifanya kazi vile ambavyo walitarajia itatokea,” Kalt amesema.
Hivi leo, wakati Wamarekani wakitafakari kuporomoka kwa siasa kufuatia ghasia za uvamizi Jumatano katika kitovu cha madaraka ya katiba, baadhi ya wataalam wanatafakari iwapo Trump, katika siku zake za mwisho madarakani, anaweza kutoa msamaha wa kiholela kwa wale wote waliojihusisha na ghasia hizo.
Uwezekano wa misamaha hiyo tayari unatoa msukumo katika Baraza la Wawakilishi la Marekani kujaribu kumuondoa madarakani Trump kabla ya kipindi chake cha urais kumalizika Januari 20.
Wakati maelezo mapya juu ya kifo cha afisa wa polisi wa Bunge la Marekani – ambaye ameripotiwa kuuawa na genge hilo – kutoa msamaha wowote kutawakasirisha sana watu, wataalam wanasema hakuna kizuizi cha sheria kinachomzuia Trump kutoa msamaha huo.