Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:09

Maoni : Asilimia 57 ya Wamarekani wataka Trump aondolewe madarakani


Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump

Asilimia 57 ya Wamarekani wanataka Mrepublican Rais Donald Trump haraka kuondolewa madarakani baada ya kushawishi maandamano ya wiki hii yaliyosambaa na kuwa ghasia mbaya zilizo sababisha vifo ndani ya jengo la Bunge la Marekani, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni uliofanywa na Reuters na Ipsos.

Wengi wao walikuwa wademocrat, hata hivyo, warepublican kwa hakika walikuwa wanaunga mkono Trump kuhudumu katika siku zake za mwisho, kipindi ambacho kinamalizika Januari 20.

Ukusanyaji maoni wa taifa uliofanywa Alhamisi na Ijumaa, pia umeonyesha kwamba watu saba kati ya 10 wale ambao walimpigia kura Trump mwezi Novemba walipinga hatua ya wafuasi wake wenye msimamo mkali kuvunja na kuingia ndani ya Bunge wakati wabunge walikuwa wakikutana kurasmisha ushundi wa Mdemocrat Joe Biden.

Karibu asilimia 70 ya Wamarekani waliofanyiwa utafiti pia walisema wanapinga vitendo vya Trump kuelekea vurugu za Jumatano. Katika hotuba yake mapema siku hiyo, Trump aliwahimiza maelfu ya wafuasi wake kuandamana kwenda Capitol Hill.

Vurugu zilitokea Capitol Hill, ambapo afisa wa polisi na watu wengine wanne walifariki, kwa kiasi kikubwa wote Wademocrat na Warepublican walilaani vikali.

Wafuasi wa Rais Donald Trump wakivunja uzio wakati wakiwashambulia maafisa wa polisi wanaolinda Bunge la Marekani katika maandamano yao ya kupinga kurasmishwa matokeo ya uchaguzi wa rais na Bunge la Marekani, Washington, Jan. 6, 2021.
Wafuasi wa Rais Donald Trump wakivunja uzio wakati wakiwashambulia maafisa wa polisi wanaolinda Bunge la Marekani katika maandamano yao ya kupinga kurasmishwa matokeo ya uchaguzi wa rais na Bunge la Marekani, Washington, Jan. 6, 2021.

Wademocrat katika Baraza la Wawakilishi wanapanga kuanzisha shutuma za utovu wa nidhamu hapo Jumatatu ambazo zinaweza kupelekea mara ya pili kumshtaki Trump kumuondoa madarakani, vyanzo karibu na suala hilo wamesema.

“Kama Rais haondoki ofisi haraka na kwa hiari yake, Bunge litaendelea na hatua zetu,” Spika wa Bunge, Nancy Pelosi amesema katika taarifa yake.

MIGAWANYIKO

Majibu ya umma yamegawanyika kulingana na vyama, kama inavyokuwa katika suala kuu katika enzi ya utawala wa Trump. Wakati kila mtu akilaani makabiliano ya ghasia, wito kwa Trump kuondoka madarakani kwa kiasi kikubwa yanatoka kwa Wademocrat.

Kwa jumla, Wamarekani wengi ambao wamesema wanataka Trump aondoke madarakani baada ya muhula wake kumalizika ni pamoja na watu tisa katika kila Wademocrat 10 waliofanyiwa utafiti lakini wawili tu katika kila Warepublican 10.

Kiasi cha asilimia 30 wamesema Rais ni vyema aondolewe madarakani kwa kutumia Kifungu 25 cha katiba ya Marekani, ambacho kinaruhusu Makamu Rais na Baraza la Mawaziri kumuondoa Rais kama atashindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Asilimia nyingine 14 imesema Bunge ni vyema kumshtaki kumuondoa madarakani Trump, na asilimia 13 imesema Trump ni bora ajiuzulu.

Trump, alishindwa katika uchaguzi wa Novemba 3 kwa kura milioni saba, Jumatano aliwataka wafuasi wake kuandamana kwenye Bungeni, na aliwaeleza katika hotuba yake, “hamtaweza kuichukua nchi yetu kwa udhaifu.”

Idadi ndogo ya umma wa Marekani, asilimia 12, wamesema waliukuwa wanaunga mkono hatua za watu wale ambao walishirikia katika ghasia.

Asilimia 70 ya watu wazima, wakiwemo theluthi mbili ya Warepublican na wapiga kura wa Trump, waliwaelezea washiriki kuwa ama ni “wahalifu” au “wapumbavu.” Asilimia tisa waliwaona kama “raia wenye wasi wasi” na asilimia tano waliwaita ‘wazalendo.”

Ukusanyaji maoni wa Reuters na Ipsos ulifanywa kwa njia ya mtandao, kwa kiingereza, kote nchini Marekani. Ulikusanya majibu kutoka wamarekani watu wazima, wakiwemo 339 ambao walisema walimpigia kura Trump.

Matokeo yana kiwango cha uaminifu, kipimo cha usahihi, cha asilimia nne ya pointi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG