Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:14

Maafisa polisi wanaolinda Congress wadaiwa walikataa msaada wa ulinzi


Wafuasi wa Rais Donald Trump walipovamia Bunge la Marekani Januari 6, 2021. (AP Photo/J. Scott Applewhite)
Wafuasi wa Rais Donald Trump walipovamia Bunge la Marekani Januari 6, 2021. (AP Photo/J. Scott Applewhite)

Maafisa wa polisi wanao husika kulinda usalama kwenye jengo la Bunge la Marekani mara kadhaa walikataa msaada wa ziada kabla ya maandamano ya Jumatano yaliogeuka vurugu, na kuwalazimisha wabunge kuahirisha zoezi la kurasmisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa Novemba mwaka 2020.

Shutuma hizo zimetoka kwa maafisa wa ulinzi na jeshi siku moja baada ya umati mkubwa wa wafuasi wa Rais Donald Trump wenye itikadi kali kusukuma vizuizi na maafisa wa polisi kwenye bunge na kuvamia jengo hilo.

Waziri mdogo wa ulinzi Kenneth Rapuano Alhamisi aliwaambia waandishi wa habari “ tuliwasiliana nao mara kadhaa”, akielezea majadiliano kati ya kikosi cha taifa cha ulinzi na polisi wanaolinda jengo la bunge la Marekani wiki kadhaa kabla ya ghasia.

“Tuliwauliza zaidi ya mara moja. Jibu la mwisho tulilopewa Jumapili Januari 3 ni kwamba hawatahitaji msaada wa Wizara ya Ulinzi.”

Kufuatia vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Trump kwenye bunge la Marekani, mkuu wa polisi ya kulinda usalama kwenye bunge hilo Steve Sund alijiuzulu Alhamisi jioni.

Watu wanne akiwemo afisa mmoja wa polisi walifariki kufuatia ghasia za Jumatano kwenye jengo la bunge la Marekani.

XS
SM
MD
LG