Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:26

Ushindi wa Ossoff Georgia wawapa Wademokrat udhibiti wa Baraza la Seneti


Jon Ossoff na Raphael Warnock
Jon Ossoff na Raphael Warnock

Mdemokrat Jon Ossoff amepata ushindi katika duru ya pili ya uchaguzi jimbo la Georgia Jumatano, na kuwapa Wademokrat udhibiti wa Baraza la Seneti la Marekani.

Mchungaji Raphael Warnock alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa pili wa Seneti katika jimbo la Georgia Jumanne jioni.

Warnock pia amekuwa ni mdemokrat mweusi wa kwanza kushinda nafasi ya Seneti katika jimbo la Warepublikan.

Kinyang’anyiro kati ya Ossoff na Seneta Mrepublikan David Perdue ulikuwa na ushindani wa karibu kabla ya kutangazwa kwa siku nzima.

Ossoff, msaidizi wa zamani wa bungeni na mtengenezaji wa makala ya televisheni, alijitangazia ushindi mapema Jumatano lakini wakati huo kura zilikuwa zimekaribiana kwa yeyote kutangaza ushindi.

Ushindi huo unawapa Wademokrat udhibiti kamili wa Bunge, na kuongeza uwezekano kuwa Rais mteule Joe Biden na wabunge Wademokrat wataweza kwa urahisi kutunga sheria za kuzipitisha kwa mujibu wa ajenda zao.

XS
SM
MD
LG