Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:42

Biden atarajiwa kumteua Mmarekani mweusi wa kwanza kuwa waziri wa ulinzi


Jenerali mstaafu Lloyd Austin.
Jenerali mstaafu Lloyd Austin.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kumteua Jenerali mstaafu wa jeshi Lloyd Austin kuaa waziri wa ulinzi.

Iwapo itaidhinishwa na baraza la seneti atakuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kuchukua wadhifa huo.

Austin alizaliwa mwaka wa 1953 katika jimbo la Alabama na kukulia katika jimbo jirani la Georgia.

Alihitimu masomo yake katika chuo kikuu cha jeshi cha West Point mwaka wa 1975 na akapanda vyeo katika kipindi cha miongo minne ya kazi yake.

Austin alistaafu mwaka wa 2016 na amewahi kushiriki katika operesheni za jeshi la Marekani nchini Iraq, Afghanistan, kanda ya mashariki ya kati na Asia Kusini.

Wachamnbuzi wanataja hatua hiyo ya Biden kama mwendelezo wa azma yake ya kuwa na maaafisa wa ngazi za juu kwenye serikali yake ambao ni wa misingi mchanganyiko, iwe ya rangi dini au jinsia.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG